Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 04:05

Jaji Kennedy wa Mahakama ya Juu Marekani kustaafu


Jaji Anthony Kennedy
Jaji Anthony Kennedy

Jaji Anthony Kennedy, mwenye msimamo wa kadiri katika Mahakama ya Juu Marekani, ametangaza kustaafu kwake Jumatano, akimpa Rais Donald Trump fursa aliyokuwa anaitafuta kumweka mahala pake Jaji ambaye ni mkonservative na kubadilisha muundo mzima wa mahakama ya juu kabisa ya taifa.

Kennedy, 81, ametumikia katika mahakama hiyo kwa miaka 30 na mara nyingi amepiga kura ya maamuzi katika kesi muhimu, ikiwemo zile zinazohusiana na utoaji mimba, udhibiti wa silaha na haki za kupiga kura.

Tarehe ya kustaafu kwake itaanza mwisho wa Julai 31.

Katika tamko lake, Kennedy amesema ilikuwa “ni heshima kubwa na upendeleo wa kipekee kupewa nafasi ya kutumikia taifa letu katika mahakama za serikali kuu kwa miaka 43, miaka 30 kati ya hiyo katika Mahakama ya Juu.”

Mrithi wake atakaye tajwa na Trump kuna uwezekano mkubwa atafanya jopo la majaji walio wengi kuongeza idadi ya wenye msimamo wa pamoja ambao ni makonservative katika mahakama hiyo.

Kukosekana Kennedy kutafanya mahakama hiyo igawanyike kati ya majaji waliberali wanne ambao walikuwa wameteuliwa na marais wademokrati na majaji wanne ambao waliteuliwa na Warepublikani.

Dakika kadhaa baada ya Kennedy kutangaza kustaafu kwake, Trump amesema kuwa “mara moja” ataanza kutafuta atakaye chukua nafasi ya jaji huyo, na kusema kuwa Kennedy alikuwa ni mtu mwenye “uoni mpana.”

Kennedy alikuwa ana andika maoni muhimu ya mwisho ya Mahakama ya Juu, ikiwemo uamuzi wa kipekee wa 2015 ambao ulihalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja nchini Marekani.

“Jaji Kennedy ni sauti yenye msimamo wakadiri na mwenye uamuzi wa kura katika mahakama hiyo. Atakaye chukua nafasi yake ni muhimu sana katika kuleta uwiano wa kiitikadi katika mahakama, na bila shaka ataleta msuguano,” amesema Charles Geyh, profesa katika Chuo Kikuu cha Indiana, shule ya sheria.

XS
SM
MD
LG