Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:03

Mahakama kuu imeikubali marufuku ya safari iliyotolewa na Trump 2017


Mahakama ya juu Marekani, Jumanne iliunga mkono masharti ya marufuku ya safari yaliyowekwa na utawala wa Trump kwa raia kutoka nchi tano za ki-Islam na kumpatia Rais Donald Trump ushindi katika kutekeleza moja ya sera zake kuu zenye utata.

Katika kura ya uamuzi iliyogawanyika 5 kwa 4 mahakama ya juu ilieleza kwamba rais ana mamlaka ya kikatiba chini ya sheria za uhamiaji Marekani kudhibiti safari kutoka nchi za kigeni kutokana na wasi wasi wa usalama wa taifa, kama ambavyo utawala unavyosema.

Jaji mkuu wa Marekani, John Roberts
Jaji mkuu wa Marekani, John Roberts

Jaji Mkuu wa Marekani, John Roberts alielezea mawazo ya wengi, akiandika kwamba amri ya utendaji ya Septemba 2017 kutoka kwa Rais Donald Trump, akidhibiti safari ni mamlaka machache aliyonayo ndani ya katiba chini ya sheria za uhamiaji Marekani.

Wakati huo huo jaji mkuu alipuuzia mjadala wa changamoto juu ya amri hiyo ya utendaji kutoka jimbo la Hawaii, muungano wa waislam wa Hawaii na wakazi watatu kwamba vidhibiti vya safari vilikiuka vipengele vya kanuni ya kwanza ya katiba ya Marekani ambayo inazuia kupendelea dini moja dhidi ya dini nyingine.

XS
SM
MD
LG