Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 21:21

Hotuba ya Museveni mbele ya Netanyahu yakosolewa


Rais Yoweri Museveni akimpokea mgeni wake waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika uwanja wa ndege wa kimataifa Entebbe Uganda.
Rais Yoweri Museveni akimpokea mgeni wake waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika uwanja wa ndege wa kimataifa Entebbe Uganda.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitembelea Uganda Jumatatu ikiwa ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya siku 4 katika nchi za Afrika mashariki ziara hiyo inaonekana kama jambo muhimu kwa eneo hilo ambalo hakuna kiongozi wa Israel amewahi kutembelea katika muda wa miaka 30.

Hata hivyo siku hiyo iliingiwa na doa na utata baada ya rais wa Uganda Yoweri Museveni mara kadhaa kuitaja Israel kama Palestina wakati wa hotuba yake.

Rais huyo alizungumzia operesheni ya uwanja wa ndege wa Entebbe ambapo makomando wa Israel walipookoa mateka katika uwanja wa ndege wa Entebbe baada ya ndege ya Air France kutekwa na wanamgambo wa Palestina.

Waisrael kwenye Twitter walilaani mchanganyiko huo na kusema hotuba hiyo ya rais ilikuwa ni ndefu isiyo na mpangilio na janga kubwa na kuripoti radio ya taifa ya Israel ilikata matangazo ya hotuba hiyo kabla haijamalizika.

Mpaka sasa hakuna majibu yeyote kutoka kwa waziri mkuu Bemjamin Netanyahu.

XS
SM
MD
LG