Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 05:05

Botswana yaahidi wahamiaji wote wapatiwe chanjo ya COVID -19


Wateja wamevaa barakoa kujikinga na Covid 19 katika duka la vyakula mjini Gaborone, Botswana, March 31, 2020, katika wiki za mwanzo za kuzuka kwa virusi vya corona nchini humo.r

Serikali ya Botswana imetoa uhakikisho kwa wahamiaji wasio halali nchini humo kuwa watapatiwa chanjo ya Covid 19, licha ya hapo awali baadhi yao kurejeshwa bila ya kupatiwa chanjo hiyo.

Serikali ya Botswana imesema kuwa maelfu ya wahamiaji wasio na nyaraka halati hawataachwa katika program maalum ya kuwapatia watu chanjo ya Covid 19. Ahadi hiyo ilitolewa huku kukiwa na ripoti kuwa baadhi ya wahamiaji walikataliwa kupewa chanjo kwenye vituo ambavyo vinatoa huduma hiyo.

Maelfu ya wahamiaji wasio na nyaraka halali kuishi nchini Botswana wanasema hawakupatiwa chanjo walipofika kwenye vituo ambavyo vimetengwa kwa ajili ya utoaji wa chanjo.

Lakini waziri mdogo wa Afya, Sethomo Lelatisitswe, ameliambia bunge la taifa Ijumaa, hakuna mtu ikiwemo wahamiaji ataachwa katika program ya utoaji chanjo ya Covid 19.

Amesema wanao wahamiaji ambao wamepatiwa chanjo, hata wale ambao hawana nyaraka, ikiwemo wakimbizi, wanapatiwa chanjo dhidi ya Covid 19, kwasababu kama wataachwa, hospitali nchini humo zitajaa wagonjwa, Lelatisitswe amesema.

MNbunge Dithapelo Keorapetse aliuliza katika kikao cha bunge iwapo wahamiaji wasio na nyaraka halali nao pia wataingizwa katika program ya kupatiwa chanjo.

Amesema haelewi kwanini rekodi haiwekwi kuhusu idadi ya wahamiaji azmbao wamepatiwa chanjo, ili iweze kusaidia, kuwa na habari za uhakika na kuandaa sera mahsusi kuhusu suala hili. Pia amesema wahamiaji wanahitaji kufahamu kuwa wanastahili kupatiwa chanjo.

Mkhululi Moyo ni mmoja wa maelfu ya wahamiaji kutoka nchi jirani ya Zimbabwe. Aliondoka nchini kwao ili kutafuta fursa nzuri ya kiuchumi. Moyo anasema ana furaha maafisa nchini Botswana wameielezea vyema program ya utoaji chanjo kwa wahamiaji.

Maafisa wa afya nchini humo wanasisitiza hivi sasa kuwa bila ya masharti yoyote wahamiaji watapatiwa misaada inayostahili kuhusu chanjo na matibabu.

Botswana inakadiriwa kila mwaka inawaondoa nchini takriban wahamiaji haramu 22,000 wengi wao kutoka nchini Zimbabwe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG