Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:15

Iran yadai shambulizi lililofanywa na Israel lina ajenda ya siri


Bahram Ghasemi
Bahram Ghasemi

Iran imesema sababu zilizoelezewa juu ya mashambulizi la roketi yaliofanywa na Israel dhidi ya Syria siyo za kweli na zina ajenda ya siri.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Ghasemi amesema kwamba mashambulizi ya Israel yalikiuka sheria za kimataifa za kuheshimu uhuru wa nchi na mipaka ya taifa la Syria.

Ameongeza kuwa, Syria inayo haki ya kujihami dhidi ya waliofanya mashambulizi hayo ya uchokozi.

Jeshi la Israel limeonyesha Ijumaa picha za video za vituo vya jeshi la Iran nchini Syria vilivyolengwa na ndege za kijeshi za Israel.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress ametowa wito kwa Iran na Israel kusitisha mara moja hujuma na vitendo vya uchokozi kati yao ili kuepusha mfumuko wa mzozo mkubwa katika eneo la mashariki ya kati.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman, Ijumaa, amemtaka Rais Bashar Assad kuondoa majeshi ya Iran nchini Syria, akionya kuwa uwepo wao unahatarisha usalama wa nchi yake

"Nachukuwa nafasi hii kupeleka ujumbe kwa Assad, ondosha majeshi ya Iran, mwondoshe Qasem Soleimani, na Majeshi ya Quds, hayakusaidii, wanasababisha hasara na uwepo wao utasababisha matatizo na maangamizi. Waondoe Wairani na pengine itawezekana kuwa na maisha tofauti."

Akizungumza wakati akitembelea eneo la Golan Heights linaloshikiliwa na Israel, Lieberman amesema: "Sisi hatutafuti mgogoro... Sisi hatukuenda katika mpaka wa Iran, wao wamekuja hapa."

Israel imeonya kuwa haitovumilia adui wake ambaye ni Iran kuweka jeshi lake karibu na eneo lake.

XS
SM
MD
LG