Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 13:13

Marekani yasema Iran pamoja na kusitisha progamu ya Nyuklia bado ni hatari


Rais wa Iran Hassan Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani

Serikali ya Marekani imethibitisha tena kwamba Iran inafuata makubaliano ya kimataifa ya mwaka 2015 kuhusu mipango yake ya nyuklia.

Hata hivyo makubaliano hayo Rais Donald Trump ameyaita ni makubaliano mabaya mno ambayo yameshawahi kufikiwa katika mazungumzo wakati wowote.

Chini ya sheria za Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani lazima itoe taarifa kwa bunge kila baada ya asiku 90 kuhusu namna Iran inavyotii makubaliano hayo.

Afisa wa ngazi ya juu wa kiutawala amesema kwamba wakati Iran inafuata masharti ya makubaliano kiufundi, bila shaka bado imekuwa ikikaidi umuhimu wa makubaliano hayo.

Ameongeza kuwa uongozi wa Trump unafanya kazi na washirika wake kuhakikisha inaendelea kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa na kusonga mbele.

Afisa huyo wa ngazi ya juu amewaambia waandishi wa habari Ikulu ya White House inaamini kuwa Iran bado inaendelea kuwa serikali hatari mno, na kutoa kama ushahidi vitendo vya Tehran kusaidia ugaidi, kuendeleza uadui dhidi ya Israel, mashambulizi ya mitandao dhidi ya Marekani na mambo kadhaa ya uvunjifu wa haki za binadamu.

“Vitendo hivi kwa kweli vinadhoofisha kusudio la makubaliano hayo,” amesema afisa huyo.

XS
SM
MD
LG