Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:08

ODM yatishia kuanza tena maandamano kuhusu IEBC


Bw. Musalia Mudavadi (kushoto) akiwa pamoja na kiongozi wa ODM Raila Odinga (kulia) wakihudhuria mkutano wa chama cha ODM.
Bw. Musalia Mudavadi (kushoto) akiwa pamoja na kiongozi wa ODM Raila Odinga (kulia) wakihudhuria mkutano wa chama cha ODM.

Na Kennedy Wandera

Mzozo unaonekana kutokota katika harakati za kufanyia mabadiliko Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, IEBC kati ya chama kikubwa cha upinzani ODM nchini humo kinachoongozwa na Raila Odinga na kamati ya sheria ya bunge iliyojitwika jukumu la kukusanya maoni ya wakenya ili kuikarabati tume hiyo ya uchaguzi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:09 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

ODM kinasema kitarudia maandamano ya kila wiki iwapo kamati hiyo ya kisheria ya bunge la kitaifa haitaondolewa. Huku kamati hiyo kisheria ya bunge la kitaifa inayoongozwa na mbunge wa eneo bunge la Anabkoi Samuel Chepkonga ikitarajiwa kuidhinisha ripoti kuhusu malalamishi yaliyoibuliwa dhidi ya makamishna wa IEBC na Bwana Barasa Nyukuri, sintofahamu imezuka upya kuhusu ni kamati gani inayofaa kutwikwa jukumu rasmi la kuanzisha mazungumzo kuondoa tume hiyo.

Mirengo ya Jubilee na CORD ilionekana kubuni kamati maalum ya wabunge kumi na wanne inayoongozwa na Kiraitu Murungi na James Orengo ili kupiga jeki mazungumzo yaliyoonekana kukwama na kuzua hisia kali za kisiasa nchini humo.

Hata hivyo mkanganyiko ni kuwa kamati gani iliyo na mamlaka rasmi kuidhinisha na kuendeleza mazungumzo hayo. Je, ni kamati ya kisheria ya bunge la kitaifa inayoongozwa na Chepkonga au ni ile maalum inayojumuisha wabunge kumi na wanne kutoka mirengo yote miwili?

Kupitia kwa taarifa iliyosomwa na kaimu katibu mkuu wa chama hicho Seneta Agnes Zani, ODM sasa kinatishia kurudia maandamano yake ya kila wiki iwapo kamati ya kisheria ya bunge la kitaifa haitaondolewa.

ODM kinahofia kuwa kamati hiyo ya kisheria huenda ikatumiwa vibaya na muungano wa Jubilee kuvuruga mapendekezo kuhusu kutimuliwa kwa makamishna wa IEBC. Wakati wa mkutano wa juu kabisa wa chama hicho NEC, ODM kinasema haitakaa kuona mfumo huo ulioafikiwa na vyama hivyo vya kisiasa kuhujumiwa.

Kamati hiyo ya Chepkonga ilikuwa tayari imewaita makamishna hao wa IEBC mbele yake na kuwaweka kwenye mizani kuhusu tuhuma za ufisadi na unaowakabili. Hata hivyo baadhi ya makamishna hao walionekana kufedheheshwa na mfumo wa kamati hiyo huku wakionekana kulemewa na hisia kali.

XS
SM
MD
LG