Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 23:58

Idhaa ya Kiswahili ya VOA yatimiza miaka 59


Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) Jumamosi imetimiza rasmi miaka 59 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1962.

Idhaa hii ilipoanzishwa ilikuwa na matangazo yaliyokuwa yakirekodiwa na kurushwa baadae na ilikuwa na watangazaji wachache.

Kadri miaka ilivyokwenda Idhaa ya Kiswahili inajivunia kwa kuwa na idadi kubwa ya wasikilizaji huko Afrika Mashariki na Kati na matangazo ambayo pia husikika kupitia kwenye tovuti ya voaswahili na mitandao yake ya kijamii pamoja na idadi kubwa ya watangazaji mahiri pamoja na wazalishaji.

Idhaa imepanuka kwa kuanzisha vipindi vya televisheni Duniani Leo ambacho kila siku kipo hewani na vingine ni Maisha na Afya, Washington Bureau pamoja na Zulia Jekundu.

Idhaa inalenga matangazo yake kwa msikilizaji wa kila umri kuanzia wazee hadi vijana na kuwapatia vipindi mbali mbali ambavyo vinalenga maisha ya kila siku kuanzia habari za afya, jamii,uchumi, elimu na siasa na hutoa fursa kwa wasikilizaji kutuma maoni na salaam zao. Idhaa ya Kiswahili inakusihi endelea kusikiliza matangazo yetu

XS
SM
MD
LG