Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:42

Hong Kong: Amnesty International yasahihisha taarifa yake ya awali kuhusu mwanafunzi aliyeripotiwa hajulikani aliko


Abuduwaili Abudureheman, (Picha ya Instagram).
Abuduwaili Abudureheman, (Picha ya Instagram).

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International linasema limewasiliana na mwanafunzi ambaye walieleza alikuwa hajulikani aliko baada ya kuwasili Hong Kong mapema mwezi huu. 

Shirika hilo la haki za binadamu lilitoa taarifa wiki iliyopita likisema Abuduwaili Abudureheman alikuwa hajawasikika baada ya kusafiri kwenda Hong Kong kutoka Korea Kusini Mei 10 kumtembelea rafiki yake.

Amnesty ilisema Abudureheman alituma ujumbe wa maandishi kwa rafiki yake akimueleza kwamba anahojiwa na polisi wa China baada ya kuwasili Hong Kong.

Amnesty iliishinikiza mamlaka huko Hong Kong kueleza alipo Abudureheman, wakieleza wasiwasi wao kuwa amepelekwa huko upande wa China bara “bila ya kufuata mchakato wa sharia na yuko hatarini kuweka kuzuizini kiholela na kuteswa.”

Taasisi hiyo ilitoa sahihisho Jumanne juu ya taarifa yao ya awali ikisema Abudureheman aliwasiliana nao na kuwaambia kuwa hakusafiri kwenda Hong Kong na walifarijika kuwa hivi sasa anajulikana aliko.

Mamlaka Hong Kong imetoa taarifa Jumapili ikisema madai ya Amnesty “hayana msingi na siyo ya kweli” na kuwa “yamechafua hali ya haki za binadamu” katika mji huo wa China.

China imekuwa ikishutumiwa na makundi ya haki za binadamu ya kimataifa na nchi za Magharibi kwa kuwaweka kizuizini mamilioni ya Waislamu wa kabila la Uyghur na makundi mengine ya walio wachache katika eneo nje ya mkoa wa kaskazini magharibi wa Xinjiang, wakiwatesa, kuwaondoa kizazi kwa nguvu na kuwalazimisha kufanya kazi ngumu. Marekani imetangaza rasmi vitendo vya serikali ya China huko Xinjiang kuwa “ mauaji ya kimbari.”

Amnesty ilisema katika masahihisho ya taarifa yake kuwa “itaendelea kufuatilia na kuweka rekodi ya u hali mbaya ya haki za binadamu kwa watu wa Uyghur huko China bara na nje ya nchi, pamoja na hali ya haki zaz binadamu huko Hong Kong, ambayo imezidi kuwa mbaya kwa kasi tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Usalama wa Taifa ya 2020.”

Forum

XS
SM
MD
LG