Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 11, 2024 Local time: 07:21

OIC yashutumiwa kupuuzia mateso ya Waislam wa Uyghur nchini China


Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, Kushoto, Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan Al-Saud na Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan wakihudhuria mkutano wa 48 wa Jumuiya ya OIC, Islamabad, Pakistan March 22, 2022. REUTERS/Saiyna Bashir
Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, Kushoto, Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Prince Faisal bin Farhan Al-Saud na Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan wakihudhuria mkutano wa 48 wa Jumuiya ya OIC, Islamabad, Pakistan March 22, 2022. REUTERS/Saiyna Bashir

Azimio la Marekani kuwa China imefanya uhalifu na mauaji ya kimbari dhidi ya binadamu hasa kwa  Waislamu waliowachache katika  jimbo la magharibi la  Xinjiang inaonekana kuwa na athari ndogo kwa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam yenye nchi 57...

Azimio la Marekani kuwa China imefanya uhalifu na mauaji ya kimbari dhidi ya binadamu hasa kwa Waislamu waliowachache katika jimbo la magharibi la Xinjiang inaonekana kuwa na athari ndogo kwa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam yenye nchi 57, ambapo wiki hii imempongeza Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika kikao cha juu cha umoja huo.

Akiwa amekaribishwa na Pakistan, Wang alihudhuria kikao cha 48 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC, mjini Islamabad kama mgeni rasmi na kuzungumza katika ufunguzi wa kikao hicho. Aliendelea Alhamisi kwa ziara ya kushitukiza Afghanistan, ambapo serikali ya mpito inayoongozwa na Taliban ina azma ya uwekezaji kutoka China na msaada wao.

Matukio ya mkusanyiko wa mambo yalikuwa yamewakera wanaoendesha kampeni kwa Wauighur, kikundi cha haki za binadamu chenye makao yake Washington, ambao wamelaani kitendo cha Wang kuhudhuria mkutano huo na ukimya wa OIC juu ya vitendo vya China dhidi ya jamii ya walio wachache ya Uyghur, ikiwemo unyanyasaji wa jumla katika kambi zilizoitwa ni za mafunzo mapya.

“Ilikuwa inaudhi kuona Pakistan ikimkaribisha Wang Yi kama mgeni wa heshima, wakati Waislam wa Uyghur hawana haki kujitambulisha kama Waislam na kutekeleza ibada zao," kampeni ya Uyghur imesema katika tovuti yao.

Kulingana na Hassan Askari, mchambuzi wa masuala ya kimataifa, kitendo cha Pakistan kumkaribisha waziri wa mambo ya nje wa China katika mkutano wa OIC kama mshiriki ni sehemu ya utamaduni wa OIC unaoruhusu nchi iliyokuwa mwenyeji kumkaribisha mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka nchi isiyokuwa mwanachama wa OIC.

Marekani imeishutumu China kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mkoa wa Xingjiang ulio na waislamu walio wachache magharibi mwa China, ikiwemo kufanyishwa kazi ngumu, kufungwa kizazi wanawake wao na kuwekwa kizuizini ovyo kwa zaidi ya Waislam wa Uyghur milioni 1 katika kambi mbalimbali.

Beijing imekanusha madai hayo na inasema watu wa makundi ya kikabila yote wanaishi kwa furaha huko Xinjiang.

Mkutano huo wa OIC ulizungumzia madhila ya Waislam wa Rohingya na pia wa Afghanistan, maeneo ya Wapalestina, Jammu na Kashmir na kwengineko, lakini ukapuuzia mauaji ya kimbari ya Uyghur, kampeni ya Uyghurs imesema.

Ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu pekee aliyetaja suala la Wauyghurs.

XS
SM
MD
LG