Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:32

Hatimaye mgogoro wa Tanzania na Kenya wapata ufumbuzi


Rais Uhuru Kenyatta akimkaribisha mwenzake John Magufuli ikulu Nairobi, Octoba 2016.
Rais Uhuru Kenyatta akimkaribisha mwenzake John Magufuli ikulu Nairobi, Octoba 2016.

HATIMAYE Tanzania na Kenya zimekubaliana kumaliza mgogoro wa madereva wa malori uliokuwa unafukuta katika mipaka ya nchi hizo kwa takribani wiki mbili sasa.

Ufumbuzi wa mgogoro huo umepatikana baada ya viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali katika serikali za Tanzania na Kenya kukutana mpakani eneo la Namanga.

Katika kikao hicho kilichoshirikisha mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wataalam wa sekta mbalimbali,viongozi hao wamekubaliana kuanzia sasa madereva wa malori watapimwa katika nchi zao na kupewa cheti kitakacho tambulika popote watakapo kwenda kwa muda wa siku 14.

Wakisoma makubaliano hayo Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Issack Kamwelwe na Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Machari baada ya kusaini mkataba wa makubaliano walisema kimsingi wameafikiana kuhakikisha kuwa biashara zinaendelea na pia tahadhari za kukabiliana na Corona zinaendelea.

Kuhusu utaratibu wa wananchi wa kawaida mawaziri hao wamesema jukumu hilo wamepewa wakuu wa mikoa yote iliyoko mpakani mwa nchi hizo ambao watahakikisha kuwa wananchi wenye mahitaji pande zote wanayapata bila usumbufu na wakati huo huo wakichukua tahadhari.

Wamesema katika hatua za awali wananchi watakaoguswa na mpango huu ni pamoja na wakulima ambao wamelima mazao yao upande wa pili wa mpaka ambapo sasa watawekewa utaratibu wa kuvuna mazao yao.

Wamesema baada ya tatizo lakundi hilo kutatuliwa litafuata kundi la wafugaji na pia makundi mengine.

Mkurugenzi wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki Peter Mathuki na baadhi ya wadau wamepongeza hatua hiyo huku wakiahidi kutoa ushirikiano wa kuhakikisha makubaliano hayo yanakuwa na tija pande zote.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Asiraji Mvungi, Tanzania

XS
SM
MD
LG