Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:57

Hali ya hewa kuruhusu zoezi la utafutaji miili Florida kuendelea


Hali ilivyokuwa baada ya kimbunga Elsa kusababisha mafuriko na dhoruba huko Key West, Florida, Jumanne, Julai 6, 2021. Hali hii imesababisha ugumu wa kuendelea na utafutaji wa miili ya manusura katika ajali ya jengo lililoporomoka Florida kusini.
Hali ilivyokuwa baada ya kimbunga Elsa kusababisha mafuriko na dhoruba huko Key West, Florida, Jumanne, Julai 6, 2021. Hali hii imesababisha ugumu wa kuendelea na utafutaji wa miili ya manusura katika ajali ya jengo lililoporomoka Florida kusini.

Wafanyakazi wa utafutaji wa miili na manusura katika jengo lililoporomoka huko Florida kusini wanatarajia kupata ahueni kutokana na hali mbaya ya hewa Jumatano.

Afueni ya hali ya hewa inatarajiwa Leo wakati wanaendelea kutafuta watu ambao walikuwa ndani ya jengo la makazi ambalo lilianguka takribani wiki mbili zilizopita.

Utafutaji ulilazimika kusimamishwa kwa kiasi cha saa mbili siku ya Jumanne kwa sababu ya radi na upepo mkali kutokana na kimbunga Elsa.

Dhoruba hiyo inaathiri Florida lakini imeondoka kutoka kwenye eneo la Surfside, kaskazini mwa Miami mahala lilipoanguka jengo.

Wafanyakazi walipata miili nane Jumanne na kuongeza idadi ya jumla ya vifo vya watu 36.

Meya wa Miami-Dade, Daniella Levine Cava, aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa Jumanne jioni, kwamba watu 109 bado hawajulikani walipo.

Wafanyakazi wanaendelea kufukua kwenye kifusi ambacho maafisa wanaohusika na zoezi hilo waliita mlundikano wakati wanatafuta watu na ushahidi wowote ili kusaidia kuelezea kwa nini jengo hilo lenye ghorofa 12 lilianguka hapo June 24.

XS
SM
MD
LG