Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:15

Jumla ya miili 36 imepatikana kutoka vifusi vya jengo lililoanguka Florida


Muonekano wa jengo lililoanguka huko Florida
Muonekano wa jengo lililoanguka huko Florida

Utaftaji ulilazimika kusimamishwa kwa kiasi cha saa mbili siku ya Jumanne kwa sababu ya radi, na upepo mkali kutokana na kimbunga Elsa. Dhoruba hiyo inaathiri Florida lakini imeondoka kutoka kwenye eneo la Surfside kaskazini mwa Miami mahala lilipoanguka jengo. 

Wafanyakazi wa utafutaji huko Florida kusini, nchini Marekani wanatarajia kupata auheni kutokana na hali mbaya ya hewa Jumatano wakati wanaendelea kutafuta watu ambao walikuwa ndani ya jengo la makaazi ambalo lilianguka takribani wiki mbili zilizopita.

Utaftaji ulilazimika kusimamishwa kwa kiasi cha saa mbili siku ya Jumanne kwa sababu ya radi, na upepo mkali kutokana na kimbunga Elsa. Dhoruba hiyo inaathiri Florida lakini imeondoka kutoka kwenye eneo la Surfside, kaskazini mwa Miami mahala lilipoanguka jengo.

Wafanyakazi walipata miili nane Jumanne na kuongeza idadi ya jumla ya vifo vya watu 36. Meya wa Miami-Dade, Daniella Levine Cava aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa Jumanne jioni kwamba watu 109 bado hawajulikani walipo.

Wafanyakazi wanaendelea kufukua kwenye kifusi, maafisa wanaohusika na zoezi hilo waliita mlundikano wakati wanatafuta watu na ushahidi wowote ili kusaidia kuelezea kwa nini jengo hilo lenye ghorofa 12 lilianguka hapo June 24.

XS
SM
MD
LG