Ghasia zimeongezeka katika sehemu za Sudan Kusini ambako mapambano yamechochewa na mizozo ya ndani juu ya maeneo ya malisho ya mifugo, maji, ardhi za kilimo na rasilmali nyingine ambapo mara kwa mara hali huchochea mapambano mabaya.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wiki iliyopita lilisema mzozo unaoendelea ambao ulianza mwezi Agosti katika kiijiji kimoja huko Upper Nile, tangu wakati huo umesambaa katika sehemu nyingine kwenye jimbo hilo na maeneo kadhaa kwenye majimbo ya Jonglei na Unity.