Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:15

Mapigano yaongezeka Sudan, watu 151 wameuawa


Gari lililowashwa moto wakati wa ghasia nchini Sudan Julai 18, 2022
Gari lililowashwa moto wakati wa ghasia nchini Sudan Julai 18, 2022

Watu 151 wameuawa na 86 kujeruhiwa katika mapigano katika jimbo la Blue Nile, nchini Sudan.

Licha ya kuwepo mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2020, baadhi ya makundi ya wapiganaji katika eneo la Dafur na Blue Nile pamoja na Kordofan Kusini, huku mapigano ya kikabila yakiongezeka.

Wataalam wanasema mapigano hayo yanachochewa na maswala ya umiliki wa ardhi na makundi ya wapiganaji kupata mafunzo ya kijeshi.

Mapigano yanaendelea kutishia utulivu wa Sudan ambayo inakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa na kiuchumi tangu utawala wa kijeshi ulipoingia madarakani na kuuondoa utawala wa kiraia mwaka mmoja uliopita.

Jimbo la Blue Nile limeshuhudia mapambano ya kikabila kutokana na mzozo wa ardhi tangu mwezi Julai.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba watu 149 waliuawa mwezi Septemba na wengine karibu 65,000 kuachwa bila makazi mapema mwezi huu.

Mapigano makali yameongezeka wiki iliyopita, kuanzia Oktoba 13. Watu kutoka makabila ya Hausa na Hamaj wamekuwa wakipigana katika sehemu ya Wad Almahi kwa siku kadhaa.

Walioshuhudia wamesema kwamba mapigano yameendelea hadi jumatano wiki hii, na wengi wa waliouawa ni wanawake na Watoto. Wana majeraha ya risasi na kudungwa visu.

Mapema wiki hii, mapigano yaliongezeka katika jimbo la kusini, Kordofan Magharibi, kutokana na mzozo wa umiliki wa ardhi.

Jeshi la Sudan limelaumu kundi la wapiganaji linaloongozwa na Abdelazizi al-Hilu, ambaye hakusaini mkataba wa amani. Kundi hilo hata hivyo limelaumu kikosi cha jeshi la dharura.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba watu 36,000 wamelazimika kuondoka Lagowa, ambapo mapigano makali yametokea na kwamba watu 19 wameuawa na 34 kujeruhiwa.

"Amani ya kudumu haiwezi kupatikana bila kuwepo serikali thabithi inayojali maslahi ya jamii ikiwemo usalama na kushughulikia kwa kina sababu zinazosababisha mapigano,” amesema mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa Twitter.

XS
SM
MD
LG