Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 16:19

Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara


Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:32 0:00

Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara

Ghana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi.

Mradi wa Media Foundation for West Africa

Kwaku Asante anaongoza timu ya waandishi wa habari wa kuhakiki ukweli, Fact-Check Ghana, mradi wa Media Foundation for West Africa, wenye makao yake katika mji mkuu, Accra.

Timu hiyo ina kazi ngumu ya kupambana na habari potofu na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida.

Asante anasema yeye na wanahabari wenzake wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu changamoto hiyo.

Kiongozi wa Timu ya Fact Check

Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact Check Ghana anasema:

“Kuna taarifa nyingi potofu huko nje. Ukiamka asubuhi unakuta kuna mambo mengi yanayoulizwa. Je, unaweza kuliangalia hili kwa ajili yetu? Je, hizi ni taarifa sahihi? Je, hii ni kweli? Kuna yeyote wa kutusaidia? Kisha tunafika na kusema, “ndiyo, tumeichunguza. Huu ndio ukweli. Hii si sahihi, na hii ni taarifa sahihi.”

Kuhakiki ukweli, ni kazi ambayo Asante anaipenda, kwa miaka mitano iliyopita, alifanya kazi kuwajuza raia wa Ghana na taarifa sahihi.

Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact-Check Ghana asema: “Inanipa furaha kubwa kujua kwamba unafanya kitu ambacho kinaleta matokeo mazuri na ushawishi wa moja kwa moja kwa watu, kwa sababu habari za uongo zinaweza kuwa na athari mbaya sana, tizama kipindi cha Covid 19 ambapo kulikuwa na mtiririko wa habari za uongo.”

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu

Mwanafunzi wa chuo kikuu Portia Fafali Gedza anatambua vyema kuhusu athari ya habari za uongo kwenye WhatsApp kuhusu Makamu wa Rais wa Ghana Mahamadu Bawumia kwamba alikuwa anatoa pesa taslimu.

Portia Fafali Gedza, mwanafunzi wa chuo kikuu anasema: “Mtu mmoja alinitumia kiungo cha taarifa kwamba Bawumia anagawa pesa. Nilibofya tu kwenye kiungo hicho, nikapitia mchakato wote, na ilifika mahali ambapo ilibidi nisambaze habari hiyo kwenye WhatsApp. Niliisambaza, na mwisho wa siku, sikutapa pesa. Kuna mtu alikuja kuniambia kwamba hizi habari ni za uongo, kwa hiyo nisingewaamini. Kwa sababu fikiria muda nilitumia kusambaza viungo hivyo, sikuweza kufanya chochote, na hivo, nilikuwa natumia bundle zangu, nilikuwa nasambaza kitu ambacho ni uzushi. Nilipata aibu.”

Vifaa vya Kidigitali

Asante na timu yake wanatumia vifaa vingi vya kidijitali kuchunguza habari. The InVID fake debunker ni mojawapo, inasaidia kuthibitisha chanzo cha video yoyote ambayo inachapishwa mtandaoni. Asante anasema vifaa zaidi vya kuchunguza vipo ili kusaidia.

Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact-Check Ghana asema: “Linapokuja suala la video, Invid Fake debunker imekuwa ikitusaidia kila wakati kuvuta picha ili kutusaidia kufanya ukaguzi wa video. Kuna mtandao mpya ambao unajitokeza. Geospy inachanganya mfumo wa Google kwa picha na utambulishaji wa maeneo pia inatusaidia sana.”

Timu ya FactSpace West Africa

Asante haiko peke yake katika vita hivi. Rabiu Alhassan ni mwandishi wa habari anayefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Yeye ndiye kiongozi wa timu ya FactSpace West Africa, shirika la kuhakiki ukweli linalofanya kazi kukabiliana na habari potofu kadhalika propaganda kote Afrika Magharibi.

GhanaFact ni sehemu ya shirika hilo.

Alhassan anasema kwake, kupambana na habari potofu ni zaidi ya kazi. Anajua madhara ya habari mbaya kwa watu wa kawaida, mataifa na kanda nzima ya Afrika Magharibi.

Vyumba vya Habari Kuunda Madawati Kuhakiki Habari

Rabiu Alhassan, kiongozi wa timu ya Fact Space West Africa aeleza: “Hatuko mbali sana kuwaona watu wenye nia mbaya wakifuatilia kile kinachofanyika nchini, kubaini makosa makubwa na kujaribu kutumia hilo. Sababu tunajaribu kutumia uwezo wetu mdogo kuleta matokeo mazuri kwa kusaidia vyumba vya habari katika kuunda madawati yao ya kuhakiki ukweli, kwa kuwasaidia wanahabari kuwa na ujuzi wa kutosha kutambua habari potofu na kukabiliana na kampeni za taarifa potofu.”

Alhassan na timu yake wanategemea vifaa kadhaa vya kidijitali kuwasaidia katika kazi yao. Kifaa marufu kati ya hivyo ni kutafuta baadhi ya picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Ana matumaini kwamba kuhakiki ukweli inaweza kupunguza taarifa potofu.

Vijana Wengi Mitandaoni

Rabiu Alhassan, kiongozi wa timu ya FactSpace West Africa:

“Tunaona vijana wengi zaidi mtandaoni, na kuna hamu zaidi ya wadau mbalimbali kuweza kudhibiti simulizi, kama tulivyoona kwenye vyombo vya habari vya kawaida pia mtandaoni. Kwa hivyo, kazi yetu imekuwa muhimu sana. Kuna matumaini makubwa katika siku zijazo, na tuna imani kwamba tutachangia kwa uwezo wetu mdogo kukabiliana na matatizo ya habari, sio tu nchini Ghana bali katika bara zima.”

Alhassan sasa anawashauri vijana wanaochunguza ukweli kujiunga na timu yake.

Timu ya FactSpace West Africa

Gifty Tracy Aminu, kutoka timu ya FactSpace West Africa: “Nimefurahishwa na ukweli kwamba ninaweza kuwaambia wananchi zaidi ya kile ambacho mtu amesema au zaidi ya kile kilichoripotiwa, nimeweza kuchunguza kwa undani kujua kwamba jambo hilo ni ukweli au la.”

Mradi wa Fact-Check Ghana

Kwenye mradi wa Fact-Check Ghana, Asante anashiriki ujuzi wake na wanahabari vijana kuhakikisha kupambana na taarifa potofu inakuwa msingi wa kazi ya mwandishi wa habari.

Thelma Amedeku, kutoka timu ya Fact-Check Ghana

“Ilikuwa mara ya kwanza kufanya kazi ya kuhakiki ukweli, kutoka kwenye program ya NGIJ( Next Generation Investigative Journalism), na sasa nafanya kazi na mradi wa Fact-Check Ghana. Kwaku amekuwa na mchango mkubwa sana katika safari yangu kama mhakiki kwa sababu tangu kwenye program hiyo, alikuwa mkufunzi wangu na sasa ni mhariri wangu, kwa hivyo amekuwa na mchango mkubwa sana katika safari yangu kwenye mradi wa fact checker.”

Imetayarishwa na Mwandishi wa VOA Isaac Kaledzi, Accra, Ghana.

Forum

XS
SM
MD
LG