Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:31

Usambazaji wa habari potofu katika uandishi wa habari ni 'dhambi", asema Papa Francis


Papa Francis akiongoza ibada ya Angelus, Vatican, Agosti 13, 2023
Papa Francis akiongoza ibada ya Angelus, Vatican, Agosti 13, 2023

Papa Francis Jumamosi amekemea usambazaji wa “habari potofu na za uongo” katika juhudi za kushawishi maoni ya umma kama kosa kubwa katika misingi ya uandishi wa habari

“Taarifa za kupotosha ni moja kati ya dhambi za kwanza, acha tuseme makosa ya uandishi wa habari,” Francis aliwaambia waandishi wa habari wa Italy katika hafla ya kutoa tuzo ya uandishi wa habari huko Vatican.

Akichukuliwa kuwa mzungumzaji mahiri, Papa alirejea neno “dhambi” ili kuorodhesha kile alichokiita maovu manne ya vyombo vya habari, kulingana na taarifa ya Vatican iliyotafsiriwa kuhusu maoni yake.

“Taarifa potofu, wakati uandishi wa habari hautoi taarifa sahihi au unaarifu vibaya, unakashifu, wakati mwingine hii hutumiwa, ni kashfa ambayo ni tofauti na kashfa lakini inaharibu, na kosa la nne ni kupenda kashfa,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG