Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 12:15

Rais Museveni alisamehe gazeti la Red Pepper


Gazeti la Red Pepper

Gazeti mashuhuri zaidi la udaku nchini Uganda linatarajiwa kurudi mitaani muda siyo mrefu baada ya uongozi wake wa juu kuahidi kufuata weledi na hivyo kupewa msamaha na rais Jumanne jioni.

Wahariri wanane na wakurugenzi wa gazeti la Red Pepper walikuwa hapo awali wametuhumiwa na kosa la uhaini na baadae tuhuma ya kumharibia Rais Yoweri Museveni heshima yake na wakuu wengine kufuatia chapisho lenye habari iliyokuwa inadai kuwa Uganda ilikuwa inapanga kuipindua serikali ya Rwanda.

“Baada ya mkutano na Rais Museveni Ikulu, Entebbe Jumanne usiku, aliwasamehe wakurugenzi wa kampuni hiyo na wahariri wake wa ngazi ya juu na kuahidi kuamuru polisi kuondoka katika jengo la makao makuu ya Pepper walilokuwa wanalizingira,” mchapishaji alisema katika tamko lake.

“Wakati wa mkutano huo ikulu, Rais aliwaonya wakurugenzi na wahariri kuacha kutokuwa makini na kufuata weledi wa kazi yao wakati wanapopasha habari umma. Wakurugenzi hao walimuahidi rais na taifa kufanya mageuzi makubwa na kuchapisha habari kwa weledi wa hali ya juu,” gazeti la Red Pepper limesema.

Tamko hilo pia limeongeza kuwa gazeti hilo la udaku, ambalo limejikita katika umbeya na kuibua matukio ya kisiasa, “litakuwa mitaani mara nyingine tena” baada ya kupotea kwa zaidi ya miezi miwili tangu polisi walipovamia ofisi zao Novemba 2017.

Msemaji wa rais amethibitisha Jumanne kufanyika mkutano huo Jumanne akisema gazeti la Red Pepper lilikuwa limeruhusiwa kurudi mitaani baada ya “ kuomba radhi kwa taifa”.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG