Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 12:01

Filamu ya "Barbie" yapigwa marufuku Algeria


Wanasesere wa Barbie huko Duesseldorf, Ujerumani. Julai 25, 2023. Picha na Ina FASSBENDER / AFP.
Wanasesere wa Barbie huko Duesseldorf, Ujerumani. Julai 25, 2023. Picha na Ina FASSBENDER / AFP.

Algeria imeiondoa filamu ya "Barbie" kutoka kwenye sinema zake baada ya kuripotiwa kukiuka maadili, na hivyo kujiunga na idadi inayoyoongezeka ya nchi za Kiarabu ambazo zimeipiga marufuku filamu hiyo iliyopata umaarufu mkubwa duniani.

Barbie, ambayo inaongoza duniani kwa kuingiza mapato ya dola bilioni 1.2, ilianza kuonyeshwa nchini Algeria Julai 19 kabla ya kuondolewa kwenye ratiba zao siku ya Jumapili bila maelezo.

Msambazaji wa filamu hiyo katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini pia ametangaza kuondolewa kwake bila kutoa sababu.

Tovuti ya habari za mtandaoni ya 24H Algerie imesema filamu hiyo iliondolewa kwa kuwa “inakiuka maadili", ikielezea vyanzo vinavyolifahamu suala hilo vizuri.

"Algeria imeingia katika malumbano kuhusu Barbie kutokana na sinema hiyo kuonyesha na matukio yaliyokusudiwa kwa hadhira ya watu wazima" na dokezo la ushoga, tovuti ya habari ya TSA iliripoti.

TSA imesema filamu hiyo "iliondolewa kwa kutumia uangalifu na busara", Ingawa sinema hiyo ilitarajiwa sana na jumuiya za LGBTQ duniani kote, filamu haionyeshi waziwazi mahusiano ya jinsia moja au mandhari ya ajabu.

Wanasesere wa Barbie katika "kliniki ya Barbie" huko Ujerumani magharibi Julai 25, 2023. Picha na Ina FASSBENDER / AFP.
Wanasesere wa Barbie katika "kliniki ya Barbie" huko Ujerumani magharibi Julai 25, 2023. Picha na Ina FASSBENDER / AFP.

Wizara ya utamaduni ya Algeria, ambayo kwa kawaida hutangaza upigaji marufuku wa filamu na kutoa sababu zake, hadi sasa imekaa kimya.

Uamuzi wa kusitisha kuonyeshwa kwa filamu hiyo ya Barbie nchini unafuatia hatua kama hizo zilizochukuliwa na nchi zilizopo katika eneo hilo.

Kuwait iliipiga marufuku filamu hiyo siku ya Alhamisi kutokana na wasiwasi uliojitokeza kuhusu "maadili ya umma", maafisa walisema.

Waziri wa Utamaduni wa Lebanon alisema aliiomba mamlaka kuipiga marufuku filamu ya Barbie siku moja kabla ya kudaiwa "kuhamasisha ushoga", huku kauli za kupinga LGBTQ zikiongezeka katika moja ya nchi huru zaidi ya Mashariki ya Kati.

Hata hivyo filamu hiyo bado haijaonyeshwa nchini Qatar, na pia haijatoa tangazo rasmi kuhusu suala hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG