Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:08

Mtoto wa Tshisekedi ateuliwa kuongoza upinzani DRC


Felix Tshisekedi, (kushoto) akiwa pamoja na msemaji wa chama cha UDPS Jean-Marc Kabund,mjini Kinshasa, DRC 28 octobre 2016. (VOA/Top Congo)
Felix Tshisekedi, (kushoto) akiwa pamoja na msemaji wa chama cha UDPS Jean-Marc Kabund,mjini Kinshasa, DRC 28 octobre 2016. (VOA/Top Congo)

Felix Tshisekedi ameteuliwa kuwa kiongozi wa muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA kikao cha upinzani kwa ajili ya uteuzi huo kilidumu siku ya Alhamisi usiku kucha.

Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo umesema umesema uteuzi huo ulifanyika kwa ridhaa ya vyama vyote.

Lakini mwandishi wetu ameripoti kuwa uteuzi wa baraza la wazee la Rassemblement na kamati ya ufuatiliaji wa mkataba wa kisiasa hadi uchaguzi mkuu, umekumbwa na utata na kutishia mpasuko.

Lakini uteuzi huo umezusha upinzani mkali ndani ya Rassemblement wakati baadhi ya wanasiasa wakisema kuwa uteuzi huo wa wakilishi katika baraza hilo hauna uzito wowote.

“Hayo yote wanayofanya hayana uzito wowote, hatukubali watu ambao hawana rikodi yoyote kwenye upinzani kuja kuchukua nafasi hizo.

XS
SM
MD
LG