Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 09:59

Familia za Waukraine zinashinikiza kurejeshwa kwa wapendwa wao wanaoshikiliwa Russia


FILE - Raia wa Ukraine anayejitolea Oleksandr Osetynskyi, 44 akiwa amebeba bendera ya Ukraine na kuwaongoza mamia ya wakimbizi waliokimbia Ukraine wakati wakiwasili mpakani huko Medyka, Poland, Machi 7, 2022.
FILE - Raia wa Ukraine anayejitolea Oleksandr Osetynskyi, 44 akiwa amebeba bendera ya Ukraine na kuwaongoza mamia ya wakimbizi waliokimbia Ukraine wakati wakiwasili mpakani huko Medyka, Poland, Machi 7, 2022.

Mykola na Natalia  Navrotsky wanatoka katika mji mdogo wa Dymer, kiasi cha  kilomita 48 kutoka Kyiv.

Mara ya mwisho walimuona mtoto wao wa kiume, Oleksandr, Machi 2022, wakati mtu huyo mwenye umri wa miaka 33 akijaribu kuiondoa familia yake kutoka katika mkoa uliovamiwa na Russia.

“Mtoto wetu alichukuliwa na majeshi ya serikali kuu ya Russia katika kituo cha ukaguzi cha Dymer wakati akiendesha gari akiwa na mkewe na mtoto wake kutoka kijiji hicho cha Havrylivka kwenda Hlibivka.

Waligindua kitu kama simu ya mkononi na kumtia ndani. Mke wake na mtoto wake wa kiume waliachiliwa, walifika hapa wakati wa usiku uliokuwa na baridi kali, Navotskys alisema.

Mji wa Dymer na miji mingine jirani katika mkoa wa Kyiv ilivamiwa na majeshi ya Russia Februari 26, 2022. Vizuizi vya barabarani, ukamataji holela na kuteswa kwa wafungwa wa kiraia ulifuatia haraka, kulingana na wakazi na maafisa wa Ukraine.

“Walimchukua yeye Machi 8, 2022, walikuwa wanampiga vibaya sana, walimtesa, na baadae kumpeleka Hostomel,” Mykola na Natalia Navrotsky alisema katika mahojiano, wakieleza kile walichoelezwa na jirani ambaye naye alishikiliwa kiholela katika gereza mpaka majeshi ya Russia yaliporudi nyuma.

Kulingana na Shirika la Media Initiative for Human Rights (MIHR), ambalo limeundwa na waandishi wa habari wa Ukraine ambao linachunguza madai ya uhalifu wa kivita yanayofanywa na Russia nchini Ukraine, Majeshi ya Russia yalianzisha jela mbili huko Dymer, mji wenye takriban watu 7,000.

Katika muda unaozidi mwezi mmoja wa uvamizi huo, kiasi cha wafungwa 500 walipitia katika magereza hayo na kiasi cha watu 50 kati yao bado wanashikiliwa na Russia.

Navrotsky aliwekwa katika jengo la kiwanda huko Dymer mpaka pale majeshi ya Russia yaliyokuwa yanaondoka katika eneo yalipompeleka Belarus, na hatimaye Russia, wazazi wake walisema, kufuatia taarifa zilizotumwa na wafungwa wa kivita wa jeshi la Ukraine waliokuwa wamekutana na mtoto wao katika gereza huko Russia.

“Kijana bado anashikiliwa. Hivi sasa, hatujui kitu chochote kuhusu hali yake, nini kimemtokea, au vipi na lini atarejea nyumbani – hatujui chochote kabisa.” Navrotskys alisema.

Mtoto wao wa kiume aliweza kutuma taarifa kwao kupitia Shirika la Msalaba Mwekundu mwaka jana.

“Tunajua kuhusu mahali alipo kuanzia Agosti 29 [2022] – kulikuwa na ujumbe wa maandishi ulioandikw amwaka mmoja uliopita, mwezi Aprili: “Habari. Bado niko hai na afya nzuri, kila kitu kiko sawa,’” Navrotskys aliiambia VOA.

Wanakadiria kuwa mpaka sasa hajahamishwa tangu alipotuma ujumbe wa maandishi.

Wakazi wengine kadhaa wa Dymer, ambao ndugu zao walitoweka wakati wa uvamizi wa Russia, walieleza visa vinavyofanana na habari hii.

Forum

XS
SM
MD
LG