Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 21:11

Harakati za kuhamasisha umuhimu wa misaada ya Marekani kwa Ukraine kuanzishwa Washington


Baadhi ya vifaru vya kijeshi vilivyotumwa awali na Marekani kwa Ukraine. Picha ya maktaba

Shirika jipya hapa Washington DC linalenga kutumia dola milioni 2 kwenye kampeni ya matangazo inayolenga kuhamasisha wabunge wa Repablikan kuunga mkono msaada wa Marekani kwa Ukraine.

Kampeni hiyo inaanzishwa wakati kukiwa na malumbano makali bungeni ambayo huenda yakahatarisha utoaji wa misaada kwa taifa hilo linapoendelea kukabiliana na uvamizi wa Russia. Mradi huo kwa jina Repablican for Ukraine, upo chini ya shirika kubwa la Defending Democracy Together, likiongozwa na mkusanya takwimu mrepablikan Sarah Longwell, na mkonsavative Bill Kristol.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati uungaji mkono wa msaada wa Marekani kwa Ukraine ukishuka miongoni mwa wapiga kura wa Marekani na hasa wale wa Repablikan wa kikonsavative. Shirika hilo limepanga kutumia video kutoka kwa zaidi ya wapiga kura 50 warepablikan kutoka kote Marekani, wakieleza sababu zao za kuendelea kuunga mkono juhudi za Marekani za kutoa msaada kwa Ukraine.

Waripablikan wanaounga mkono Ukraine watatumia video hizo kwenye matangazo yanayolenga wapiga kura wa repablikan pamoja na wabunge. Huku pia wakizionyesha wakati wa mdahalo wa kwanza wa wawania wa urais, kutoka chama hicho, wiki ijayo.

Forum

XS
SM
MD
LG