Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 14:14

Hisia za familia ya George Floyd : 'Tutaendelea kusimama imara'


Wanafamilia ya George Floyd : Kaka yake, Philonise (Kushoto) na Terrence (Kati), Mpya wake Brandon Williams (Kulia), Mchungaji Al Sharpton (wapili kulia) wakimshukuru Mungu baada ya hukumu dhidi ya Afisa wa polisi mzungu wa Minneapolis Derek Chauvin,
Wanafamilia ya George Floyd : Kaka yake, Philonise (Kushoto) na Terrence (Kati), Mpya wake Brandon Williams (Kulia), Mchungaji Al Sharpton (wapili kulia) wakimshukuru Mungu baada ya hukumu dhidi ya Afisa wa polisi mzungu wa Minneapolis Derek Chauvin,

Baadhi ya ndugu wa familia ya George Floyd Ijumaa wamesema hukumu ya mauaji ya kifungo cha miaka 22 na nusu aliyopewa Derek Chauvin kwa kifo cha ndugu yao ilikuwa haitoshelezi.

Wanafamilia wengine walieleza matumaini kuwa hukumu hiyo itakuwa ni kiini cha mabadiliko.

Mmoja wa kaka zake Floyd, Rodney Floyd, ameiita hukumu hiyo ni “kumpiga kofi mhalifu kwenye kiganja.”

“Sisi tunaumia kwa kifungo cha maisha kwa kumpoteza ndugu yetu maishani, na hilo linaniumiza hadi mwisho wangu duniani,” amesema

Ndugu mwengine, Terrence Floyd, amesema “alikuwa na mashaka juu ya hukumu hiyo” mpaka alipoota na kumuona baba yake.

“Najua baba yangu alikuwa akisema, ‘Uko vizuri, yeye yuko vizuri, endelea kufanya unacho kifanya. Kwa ajili yangu na ndugu yako, kwa ajili ya jina lako,”’ alisema. “Tuko imara kwa ajili ya Floyd, na tutaendelea kuwa imara.”

Bridgett Floyd, dada ya George Floyd na muasisi wa Taasisi ya Kumbukumbu ya George Floyd, amesema hukumu hiyo “inaonyesha hatua dhidi ya ukatili unaofanywa na polisi hatimaye unachukuliwa hatua ipasavyo.”

XS
SM
MD
LG