Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:07

Mauaji ya Floyd : Derek Chauvin ahukumiwa miaka 22 jela


Jennifer Starr Dodd, katikati na wanaomuunga mkono Floyd wakifurahia hukumu iliyotolewa dhidi ya afisa wa zamani wa Minneapolis Derek Chauvin kwa mauaji ya George Floyd, Minneapolis, June 25, 2021.
Jennifer Starr Dodd, katikati na wanaomuunga mkono Floyd wakifurahia hukumu iliyotolewa dhidi ya afisa wa zamani wa Minneapolis Derek Chauvin kwa mauaji ya George Floyd, Minneapolis, June 25, 2021.

Rais Joe Biden amesema, kifungo alichopewa Chauvin kinastahiki kulingana na masharti yaliyopendekezwa, ingawa hakufahamu kwa kina jinsi uamuzi huo ulivyochukuliwa.

Afisa wa zamani wa polisi wa Minneapolis Derek Chauvin amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 22 na nusu jela kwa kosa la mauaji ya George Floyd 2020.

Waendesha mashtaka wametaka apewe hukumu ya miaka 30, na wakili wa Chauvin ametaka aachiwe huru. Chauvin alihukumiwa Aprili kwa mauaji kwa kukusudia, na mauaji bila ya kukusudia.

Kisheria, Chauvin alikabiliwa na kifungo hadi miaka 40 jela kwa mauaji ya kukusudia, na hadi miaka 25 kwa mauaji ya kiwango cha pili na hadi miaka kumi mauaji bila ya kukusudia.

Kutokana na kwamba Chauvin hana rekodi ya uhalifu wowote kabla ya kitendo hicho, muongozo wa sheria wa jimbo unasema, kwa makosa aliyoyafanya ya mauaji na mauaji bila ya kukusudia ni miaka 12 na nusu. Jaji Peter Cahill alikuwa na uwezo wa kutoa hukumu kati ya miaka 10 na miezi nane na miaka 15 kwa kila kosa.

Ben Crum wakili wa familia ya Floyd akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu anasema "leo ni siku inayotoa nafasi kwa mabadiliko Marekani. Hichi ni kifungo kirefu kabisa kuwahi kupewa afisa wa polisi wa Minnesota."

Naye mwanasheria mkuu wa Minnesota Kieth Ellison anasema hukumu hiyo haitoshi, bali inawapa uwezo wa kutafakari na kutambua kuwa huu ni wakati wa kufanyika mageuzi ya dhati ya kijamii kuelekea utendaji wa usawa kwa watu wote mbele ya sheria.

XS
SM
MD
LG