Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:55

EU yahofia Niger kuifuta sheria ya usafirishaji haramu wa wahamiaji


Wahamiaji kutoka Afrika
Wahamiaji kutoka Afrika

Tume ya Umoja wa Ulaya ilionyesha wasiwasi wake siku ya Jumanne juu ya serikali ya kijeshi ya Niger kufuta sheria ya usafirishaji wahamiaji, ikisema inaweza kuongeza idadi ya watu wanaojaribu kufika Ulaya kinyume na utaratibu.

"Nina wasiwasi sana kuhusiana na hali ilivyo sasa, na kuna hatari kubwa kwamba hii itasababisha vifo vipya jangwani," kamishna wa masuala ya ndani wa Umoja wa Ulaya Ylva Johansson alisema, akiizungumzia Sahara.

Alisema "inaweza pia kummanisha watu wengi zaidi kuja Libya, kwa mfano, na kisha labda kujaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kwenda EU".

Mkuu wa serikali ya kijeshi ya Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, Jumamosi alitia saini amri ya kufuta sheria ya 2015, ambayo ilikuwa inataka kupunguza idadi ya raia kutoka Afrika Magharibi wanaosafiri kupitia Sahara na kisha kuelekea Algeria au Libya kwa nia ya kufika Ulaya. .

Sheria hiyo, iliyopangwa chini ya serikali ya awali ya kiraia, ilikuwa imeungwa mkono na pesa za EU.

Ilihusisha kuongezeka kwa ufuatiliaji wa jangwani, ambako wahamiaji wengi hujaribu kulikwepa kwa kutumia njia mbadala hatari zaidi.

Brussels imelaani mapinduzi ya Julai 26, wakati jeshi lilipoiondoa serikali ya kiraia na kumweka kizuizini rais mteule Mohamed Bazoum katika makazi yake.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG