Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 16, 2024 Local time: 08:35

EU kutoa msaada wa muda mfupi wa dola bilioni 1.7 kwa Misri ili kuinua uchumi wake


Mkuu wa EU Ursula von der Leyen, kushoto, na Rais Abdel Fattah al Sisi.
Mkuu wa EU Ursula von der Leyen, kushoto, na Rais Abdel Fattah al Sisi.

Umoja wa Ulaya umesema Ijumaa kuwa utaipatia Misri dola bilioni 1.7 kama msaada wa muda mfupi ili kuisaidia nchi hiyo kujenga uchumi wake.

Misri mwezi uliopita ilikubali kuongezewa msaada wa dola bilioni 8 na shirika la Kimataifa la Fedha Duniani IFM ikiwa ni pamoja na mpango wa EU wenye thamani ya mabilioni ya dola ili kuboresha ushirikiano na kuisaidia kuzuia uhamiaji, wakati ikipambana na matatizo ya muda mrefu ya uchumi yanayohusishwa na uhaba wa fedha za kigeni.

Msaada wa euro bilioni 1 wa muda mfupi ni sehemu ya msaada mkubwa ambao ni mikopo wy euro bilioni 5 EU kwa taifa hilo. Euro nyingine bilioni 4 zilizobaki zitatolewa kama msaada wa muda mrefu kuanzia mwaka huu hadi 2027, lakini ni lazima uidhinishwe na mataifa yote 27 wanachama wa EU.

Msaada huo unalenga kuisaidia Misri ambayo hali ya kifedha ya Cairo ni mbaya sana na ina mahitaji ya kifedha, hasa kutokana na kuzuka kwa vita vya Gaza, pamoja na mashambulizi ya wa Houthi kwenye bahari ya Sham. Hata hivyo Misri imepewa masharti kwamba ni lazima ipige hatua kuheshimu demokrasia ikiwa ni pamoja na bunge lenye vyama tofauti vya siasa na utawala wa sheria na kutoa dhamana ya kuheshimu haki za binadamu, taarifa hiyo imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG