Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 22:14

DRC: Tshisekedi ameagiza kusajiliwa maelfu ya wanajeshi kupambana na M23


Rais wa DRC Felix Tshisekedi (kushoto) na rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia)
Rais wa DRC Felix Tshisekedi (kushoto) na rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia)

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amewaelekeza viongozi wa jeshi la nchi hiyo kufungua kambi kadhaa za mafunzo ya kijeshi kote nchini humo, kwa matayarisho ya kusajili idadi kubwa ya wanajeshi kupambana na kundi la waasi la M23 na makundi mengine ya waasi Kivu kaskazini.

Katika hotuba yake kwa taifa Alhamisi usiku, Tshisekedi ametoa wito kwa vijana wa DRC kujiunga na jeshi, akisema kwamba vita ambavyo vimelazimishwa ndani ya DRC, akisisitiza kuwa vita hivyo vimepangwa na jirani yake, Rwanda.

Tshisekedi amewaambia raia wote wa DRC kuachana na siasa kwa sasa na kulinda taifa lao kwa njia zote.

Ameeleza yaliyojadiliwa katika mikutano ya Angola, Nairobi na New York, akisema kwamba makubaliano ni kwamba waasi wa M23 waache mapigano, na kuondoka Bunagana, lakini waasi wamekataa kuheshimu makubaliano hayo.

Amesema kwamba ameamua vita kwa sababu diplomasia inaonekana imefeli.

“Kujitolea kwetu kusuluhisha mgogoro huu kwa njia ya amani sio ishara ya udhaifu au kwamba tumeshindwa kuanzisha vita dhidi ya watu wanaoendelea kuhujumu subira yetu,” amesema Tshisekedi.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba zaidi ya watu 200,000 wamekoseshwa makazi kutokana na mapigano ya makundi ya waasi hasa kundi la M23 ambalo linadai kwamba linawalinda raia dhidi ya mashambulizi ya kundi la wapiganaji la FDLR ambalo serikali ya Rwanda inadai kwamba linapanga kutatiza usalama wa Rwanda.

XS
SM
MD
LG