Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:28

Rais Donald Trump amteua Jaji Neil Gorsuch kujaza nafasi Mahakama Kuu


Rais Trump (K) ampongeza Jaji mteule Neil Gorsuch
Rais Trump (K) ampongeza Jaji mteule Neil Gorsuch

Rais Donald Trump amemteua Jaji wa mahakama ya rufaa ya serikali kuu Colorado, Neil Gorsuch kuwa jaji wa Mahakama Kuu ya Marekani.

Trump alijitokeza mbele ya kamera za televisheni katika ikulu ya White House Jumanne usiku kumtabulisha Gorsuch, akimwita ni jaji ambaye "taifa linamuhitajia vibaya sana," na kumwagia sifa kwamba shahada zake hazina utata kabisa.

Gorsuch ana umahiri mkubwa na elimu yake ya kisheria haifanani na yeyote na ana moyo wa kizalendo kutafsiri Katiba kama ilivyoandikwa," rais amesema.

Lakini wachambuzi wa kisiasa wamesema kuwa matakwa ya Warepublikan yametimia baada ya rais wa chama chao kushinda uchaguzi wa Novemba 2016 na hivyo kupata nafasi ya kufanya uteuzi huu hivi leo, japokuwa wanafikiri kutakuwa na mvutano mkubwa katika kuwashawishi wademokrati kumpitisha katika Baraza la Seneti.

Baadhi ya wachambuzi wamedai kuwa Warepublikan wameichukua nafasi ya mteule wa Obama, Jaji Merrick Garland jambo ambalo wameliita ni dhulma ya wazi.

Chaguo la Obama

Jaji Merrick Garland
Jaji Merrick Garland

​Nafasi hiyo iliyoachwa wazi baada ya kifo cha ghafla cha Jaji Scalia Februari 13 , 2016 ambacho kilisababisha upungufu katika mahakama kuu yenye majaji tisa, lakini pia mvutano wa kisiasa baina ya Rais wa zamani Barack Obama, Mdemokrat na Baraza la Seneti lililokuwa linadhibitiwa na Warepublikan.

Saa chache baada ya kufariki kwa Scalia, kiongozi wa Warepublikan katika Seneti, Mitch McConnell alisema "nafasi hiyo isijazwe mpaka apatikane rais mpya" na akaahidi kwamba seneti haitaitisha kikao cha kuidhinisha uteuzi wa Obama.

XS
SM
MD
LG