Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 02:37

Diamond Platnumz aonyesha mfano kwa kizazi kipya


Diamond Platnumz
Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Diamond Platnumz amezikonga nyoyo za mamia ya wakazi wa Tandale eneo alilozaliwa na kuishi, kabla ya kuhama eneo hilo baada ya kuanza harakati za muziki mwaka 2009.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa watu hao walio jitokeza kwa wingi Uwanja wa Magunia katika mfululizo wa nyota huyo wa Bongo Fleva kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa bima ya afya, mikopo na zawadi mbalimbali.

Diamond aliyataja mambo saba ambayo ameamua kuwafanyia wakazi wa kitongoji cha Tandale, jijini Dar es Salaam katika kusherekea kumbukumbu muhimu katika maisha yake.

Ni pamoja na kuzungumza na vijana katika uwanja wa Tandale Maguniani ambapo ameipa jina la ‘Thank you Tandale”.

Pia kugawa mikopo kwa kina mama, kutoa bima ya afya kwa watoto, kugawa bodaboda kwa vijana, kukarabati shule zote za msingi za Tandale akianza na ile aliyosoma, kuchinja ng’ombe nyumbani alikozaliwa na kula na Wanatandale na siku ya Jumapili kufanya sherehe kubwa na marafiki zake katika boti ya kifahari.

Shughuli za maandalizi za mkutano wake zilizohusisha kufungwa jukwaa, vinywaji, muziki zitagharimu zaidi ya Sh 5 milioni.

Katika mahojiano hayo na vyombo vya habari aliahidi kutoa kadi za bima za afya kwa watoto 300, ambapo ukipiga hesabu kwa kila mmoja ni wastani wa Sh 50,400 hivyo jumla anaweza kutumia zaidi ya Sh 15. 1 milioni.

Ukiachilia mbali hilo, kwa mikopo ya biashara kwa wamama 200 ambapo kila mmoja ataondoka na Sh100,000 mpaka 200,000, hivyo kiasi cha wastani wa Sh 20 milioni zitatumika katika hili.

Kuweka matanki katika shule za msingi Tandale, ambapo lengo lake ni kuhakikisha zinakuwa na mahali pa kuhifadhia maji , kila shule atatumia si chini ya Sh 900,000.

XS
SM
MD
LG