Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 21:09

Vanessa Mdee aeleza mkataba wake na Universal Music Group unampa fursa zaidi.


Muimbaji wa kizazi kipya wa Tanzania (Bongo fleva) Vanessa Mdee.

Mwanamuziki wa muziki wa bongo flava Vanessa Mdee wa Tanzania amezungumza na Jukwaa la Vijana kueleza juu ya mkataba wake mpya na lebo ya muziki kubwa duniani ya Universal Music Group.

Akiwa ni msanii wa kizazi kipya aliyekulia katika jiji la New York anaeleza hii ni nafasi ya kupeleka muziki wake katika hatua nyingine.

Anasema mkataba wake unampa fursa ya kutambulishwa kwenye soko jipya na hauwezi kumzuia kufanya kazi zake kwa uhuru na mkataba huo bado unampa fursa ya kutengeneza muziki wake wenye vionjo vya kiafrika.

Anaendelea na maandalizi ya albam yake ya kwanza kabisa itakayotoka mwezi wa nne mwaka huu na Universal Music Group.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG