Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:51

Comey adai Trump hana 'maadili ya kuwa rais'


Mkuu wa idara ya makosa ya jinai Marekani - FB I, James Comey, aliyeondolewa madarakani na Rais Donald Trump, amesema kuwa Trump hana maadili ya kuwa rais, akiongeza upo ushahidi kidogo kuwa Trump alizuia utekelezaji wa sheria.

Comey ametoa maoni hayo katika mahojiano maalum aliofanya na kituo cha habari cha ABC, siku ya Jumapili kabla ya kutoka kitabu hicho alichokiandika ambacho kinaelezea jukumu lake katika uchunguzi wa Marekani.

Uchunguzi huo ni juu ya Russia kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016 na uchunguzi dhidi ya mgombea wa chama cha Demoktrat Hillary Clinton, katika matumizi yake ya barua pepe binafsi kikazi, na pia mazungumzo ya faragha yaliyojiri kati ya Comey na rais kabla ya kumfukuza kazi mwaka 2017.

Comey alidadisiwa na George Stephanopoulos wa kituo cha ABC kuhusu kile alichoandika akidai Trump hana maadili na hasemi ukweli, je hilo linamfanya Donald Trump kuwa hastahili kuwa rais?

Comey alijibu kuwa, ni kweli usiofichika kwamba Rais lazima awe ni mwenye kujiheshimu na mwenye kushikana na maadili ambayo ni msingi wa taifa hili. Muhimu kuliko yote ni kuwa mkweli. Rais huyu hana uwezo wa kutekeleza hilo. Hana maadili ya kuwa rais.

Trump alituma ujumbe mpya wa kumshambulia Comey masaa kadhaa baada ya mahojiano yake na ABC.

“Sitaki kuamini, James Comey anaeleza uchaguzi, ambapo Hillary asiye na maadili alikuwa anaongoza, na ilikuwa sababu katika upuuzi uliofanyika katika uchunguzi wa email za Clinton.

Kwa maneno mengine, alikuwa anafanya maamuzi kwa misingi ya ukweli kwamba alifikiri mwanamama huyo atashinda uchaguzi, na Comey alikuwa anaitaka kazi. Mpuuzi” Trump ameandika katika ujumbe wa Twitter.

“Mbabaishaji James Comey… ameemewa (siyo mahiri), na atajulikana kama Mkurugenzi dhaifu kuliko wote katika historia ya FBI akilinganishwa na wengine waliotumikia wadhifa huo.

Katika kitabu hicho Comey anamfananisha Trump na Mkuu wa kikundi cha wahalifu (Mafia) na kueleza kuwa urais wake ni kama “moto wa porini.”

Kitabu cha Comey, kinachoitwa “A Higher Loyalty,” kimeandaliwa kuchapishwa Jumanne na kimefikia kuwa karibu na vitabu bora katika soko kwa sababu ya mauzo yake kabla ya kutolewa.

XS
SM
MD
LG