Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 05:46

Marekani yapeleka ujumbe mkali kwa Russia


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley (kati) akipiga kura juu ya rasimu ya azimio iliyoandaliwa na Russia Jumanne katika hatua ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali huko Syria kwenye Umoja wa Mataifa, New York, Aprili 10, 2018.

Vikwazo vipya vitaanza kutekelezwa Jumatatu ambavyo Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa Nikki Haley alikuwa amezungumzia katika kipindi cha Televisheni ya CBS ‘Face the Nation' ili kupeleka ujumbe kwa Russia juu ya silaha za kemikali zilizotumiwa na Syria.

Haley alisema kuwa Russia imeendelea kuzuia juhudi za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kuchunguza matumizi ya silaha za kemikali yaliofanywa na Syria.

Maoni yake yamefuatia shambulizi la anga la pamoja lililofanywa Jumamosi na Marekani, Uingereza na Ufaransa likilenga miundo mbinu ya silaha za kemikali inayomilikiwa na Syria.

Katika mahojiano, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumamosi alisistiza kuwa shambulizi hilo lilotumia zaidi ya makombora 100 lilikuwa siyo hatua ya kivita, lakini ni kulipiza kisasi kwa matumizi ya silaha za kemikali yalifanywa na serikali ya Syria huko mji wa Douma April 7 na kuuwa zaidi ya watu 40 na wengine zaidi ya 100 kuathirika kiafya.

Macron pia amesema amemshawishi Rais Donald Trump kuendelea kuwepo majeshi ya Marekani huko Syria kwa kipindi kirefu. Lakini Jumapili Jioni, White House imesema kuwa utaratibu haujabadilika, Trump bado anataka majeshi ya Marekani kurudi nyumbani mapema iwezekanavyo.

Na msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders ameiambia kituo cha televisheni cha ABC wiki hii kuwa jukumu la pande tatu bado halijakamilika.

Akizungumza na mwenzie wa Iran, Rais wa Russia Vladimir Putin amesema mashambulizi kama haya yataleta machafuko katika mahusiano ya kimataifa, rai iliyopingwa na manadiplomasia mstaafu na mtafiti maarufu James Jeffrey wa Taasisi ya masuala ya sera ya Mashariki ya karibu wakati akihojiwa na Idhaa ya Sauti ya Amerika.

James Jeffrey amesema, wakati ushindi wa utawala wa Assad umethibitika kwa kiwango kikubwa, unaweza kukabiliwa na hali tete itapofikia utawala huo kuingilia maslahi ya Marekani, Uturuki na Israeli ambayo wako tayari kuyahami. Profesa wa historia wa Chuo Kikuu cha Trinity David Lesch alipoulizwa mashambulizi ya Jumamosi yalikuwa yanamafanikio gani?

Hata hivyo David Lesch amesema anaimani kuwa siyo Moscow wala Tehran wanataka Damascus itumie silaha za kemikali, kitendo ambacho kitawapa Marekani uhalali wa kuingilia kati zaidi suala la Syria.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG