Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:40

Clinton awataka Wamarekani kumchagua Obama kwa muhula wa pili


Rais wa Marekani Barack Obama (kushoto) akiungana na rais wa zamani Bill Clinton jukwani baada ya Clinton kumteuwa Obama kwa mhula wa pili huko Charlotte, North Carolina, September 5, 2012.
Rais wa Marekani Barack Obama (kushoto) akiungana na rais wa zamani Bill Clinton jukwani baada ya Clinton kumteuwa Obama kwa mhula wa pili huko Charlotte, North Carolina, September 5, 2012.
Kwa siku ya pili mfululizo chama cha Demokratik kimefanikiwa kuwahamasisha wanachama kutokana na hotuba ziliztolewa kwa ufasaha wa kisiasa Jumatano, kwamba ni muhimu na kuna haja kubwa ya kumrudisha tena madarakani Bw Obama kwa mhula wa pili.

Kiongozi aliyeleta furaha na jazba ndani ya ukumbi ni rais wa zamani Clinton aliyepokelewa kama shuja.

Katika hotuba yake aliweza kuwasababisha wajumbe kusimama mara kadhaa kumshangiria akifafanua jinsi nchi iliyokuwa kabla ya obama kuchukua madarak hadi mambo yalivo badilika na mahala nchi inabidi kuelekea.

"Ikiwa unataka jamii ya mshindi anachukua kila kitu na kila moja ajitegeme basi inabidi kumpigia kura mgombea wa Republican. lakini ikiwa unataka nchi inayo gawanya kwa pamoja mafanikio na kuajibika kwa pamoja jamii ambayo ni ya sote tuko pamoja basi inabidi kumchagua Barack Obama na Joe Biden."

Alipomaliza hotuba yake alishangiriwa kwa namna ya kipekee ambayo hakuna mjumbe yeyote alishangiriwa isipokua Bi. Michele Obama pia.

Rais Obama akajitokeza jukwani na kumpogeza Clinton kwa hotuba ambayo wachambuzi wanasema ikiwa kuna wale wenye mawazo huru ambao hawajaamuwa upande gani wa kupigia kura, basi Clinton amefanikia kuwarai wengi wao kujiunga na vuguvugu la kumrudisha madarakani Onama kwa mhula wa pili .

Hotuba hiyo ya jana imetayarisha jukwa kwa Obama Alhamisi kukubali uteuzi wake na kufafanua njia anayotaka kuiongoza nchi hii kisiasa, kiuchumi na kijamii pamoja na kutoa ujumbe na kauli mbiyu ya kampeni yake.

Wachambuzi wanatarajia hotuba yake itazingatia zaidi masuala ya kiuchumi amblo ndilo swala kuu ka kampeni ya maka huu.

Mchambuzi John Zogby, anaema ni lazima kwa Bw. Obama kutafuta njia za kutetea kile anachoeleza ni mchanganiko wa mafanikio ya uchumi.

"Suala sio jee maisha yako ni bora zaidi sasa kuliko miaka minne iliyopita. bali suala ni jee maisha yako yengelikuwa bora zaidi ikiwa upande wapili ndio uloshinda maka 2008."

Baada ya kumalizika mkutano Alhamisi awamu ya mwiso ya kampeni za uchauzi utanazaa, kukiwpo pia midahalo mitatu iliyopangwa kwa wagombea kiti cha rais.
XS
SM
MD
LG