Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:10

Mkutano mkuu wa chama cha Demokratik wafunguliwa Marekani


Ukumbi mkuu kunakofanyika mkutano wa cha cha Demokratic, Charlotte, Septembar 4.
Ukumbi mkuu kunakofanyika mkutano wa cha cha Demokratic, Charlotte, Septembar 4.
Wajumbe elfu sita wanaohudhuria mkutano huu wa chama cha Demoktarik mjini Charlotte, North Carolina wanamatarajio makubwa ya kupata muongozo kabambe ili waweze kurudi katika majimbo yao na kupambana na wajumbe wa chama cha Repbulikan ambacho kinawahamasisha wafuasi wake kufanya kila wawezalo kumondoa madarakani rais Obama na kuchukuwa udhibiti kamili wa bunge.

Kutokana na hali hiyo viongozi wa chama cha demokratik wametayarisha warsha mbali mbali na kuwapatia wajumbe wenyenafasi ya kutoa mapendekezo yao na kushiriki kwenye mjadala wa kutayarisha muongozo huo.

Muongozo huo utaidhinishwa rasmi Jumanne usiku baada ya mkutano kufunguliwa saa 5 saa za Charlotte.

Kwa mtizamo huo mkutano mkubwa wa wanawake umefanyika Jumanne asubuhi ambapo viongozi wanawake wa chama wameeleza matarajio yao na kumtaka Obama kuendelea na sera zake za mageuzi hasa upande wa haki za wanaake.

Mwenyekiti wa mkutano huu meya wa Los Angeles Antonio Villaraigosa atakae toa hotuba kuu ufunguzi alisema hotuba za siku tatu wakati wa mkutano huu zitakuwa na lengo la kuwahamasisha wademocrats kuungana na kuhakikisha Obama anachaguliwa kwa mhula wa pili.

"Tutafafanua bayana hatari zilizopo katika uchaguzi huu kuchagua kati ya mgombea anaetaka kujenga uchumi kwa ajili ya watu wa tabaka la wastani na tabaka la chini dhidi ya yule anaetaka kujenga uchumi kwaajili ya tabaka la juu. Tunahitaji kiongozi atakae atakae peleka mbele nchi na wala sio kuturudisha nyuma".'

Hivyo basi viongozi wanaotarajia kuwasilisha ujumbe huo kwa ufasaha, miongoni mwao ni marais wa zamani Bill Clinton na Jimmy Carter, na wabunge mbali mbali mashuhrui wanaofahamika kote nchini na bila shaka mke wa rais Michel, atakae zungumza Jumanne usiku.

Bi Hillary Clinton waziri wa mambo ya nchi za nje anawasli moja kwa moja kutoka ziara yake ya Asia na anatazamiwa kueleza sera za kigeni za chama hichi.

Wakati mkutano ukiendelea maandamano yanaedenelea mbali kidogo na ukumbi kutokana na usalama mkali ulowekwa karibu na ukumbi , na kundi kuu linaloongoza maandamano ni lile linalojulikana sasa kama 'Occupy Wall Street" linalotaka mageuzi makubwa yafanyike katika mfumo wa fedha na hasa kutetea maslahi ya wamaskini na kupambana na tamaa ya makampuni makubwa na maajiri wa Marekani.
XS
SM
MD
LG