Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:34

China yaweka wazi raia wa Uingereza anatumikia kifungo kwa kosa la ujasusi


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin

China imethibitisha Ijumaa kuwa mwaka 2022 ilimhukumu raia wa Uingereza kifungo cha miaka mitano kwa kosa la ujasusi. Ilikuwa ni tamko lake rasmi la kwanza kwa kesi ambayo ilikuwa haijaripotiwa hadi kufikia wiki hii.

Mahakama moja Beijing mwaka 2022 “ilimhukumu mshtakiwa wa Uingereza alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza … kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kupata taarifa za kijasusi kinyume cha sheria kwa ajili ya wahusika walioko nje ya nchi,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje Wang Wenbin alisema.

Baada ya kukata rufaa, aliongeza, hukumu yake ilibakia kama ilivyo mwezi Septemba.

Jarida la The Wall Street lilitangaza habari hizo mara ya kwanza kuhusu kesi ya Ian Stones siku ya Alhamisi. Lilisema familia yake na vyanzo vingine, vilisema kuwa mfanyabiashara huyo wa Uingereza alitoweka mwaka 2018 baada ya miongo kadhaa ya kufanya kazi nchini China.

Akiulizwa kuhusu ripoti hiyo Ijumaa, Wang, akimuelezea Stones kwa jina lake la Kichina, alisema kuwa “mahakama ilisikiliza keshi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Beijing, alisema, “ilihakikisha inampa haki mbalimbali za kisheria zinazostahili” kwa mfungwa na ilipanga maafisa wa Uingereza kumtembelea na kuhudhuria kesi yake.

“China ni nchi inayoongozwa kwa mujibu wa sheria,” Wang alisema.

“Vyombo vya mahakama vinahimiza kesi kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, kulinda haki na maslahi ya kisheria ya raia wa China na wageni,” aliongeza.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG