Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 21:59

China yashinikiza uwekezaji wa kimataifa kwenye kongamano la Davos, Uswizi


Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa kwenye mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi mjini Davos, Uswizi.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa kwenye mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi mjini Davos, Uswizi.

China ilileta ujumbe mkubwa kwenye kongamano la mwaka huu la Kimataifa la Bishara mjini Davos, Uswizi, ili kujaribu kushawishi ulimwengu kwamba uchumi huo wa pili kwa ukubwa duniani upo tayari kufanya biashara, na ni tegemeo la kutosha kuwekeza.

Hata hivyo wachambuzi wamesema kwamba hotuba ya Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jumanne, ilikuwa na mapungufu katika kushawishi wawekezaji vya kutosha. Li aliongoza ujumbe wa watu 140 kwenye kongamano hilo la siku 5, likijumuisha wanasiasa na viongozi wa kibiashara. Kwa mujibu wa mtandao wa kisiasa wa Marekani wa Politico, China ilileta hadi maafisa kumi wa ngazi ya uwaziri, wenye utaalam wa uchumi wa China kwenye kikao hicho.

Li ndiyo afisa wa ngazi ya juu zaidi wa China kuhudhuria kongamano hilo la kila mwaka tangu 2017, hatua inayoashiria umuhimu wa kikao hicho kwa Beijing.China imekuwa ikijikwamua kiuchumi baada ya janga la Covid, wakati biashara za nyumba zikishuka, vijana wengi wakiendelea kukosa ajira, pamoja na kushuka kwa upelekaji nje wa bidhaa kwa mara ya kwanza tangu 2016.

Forum

XS
SM
MD
LG