Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 14:53

China na India zatofautiana kuhusu hali ilivyo katika mipaka yake


Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu na mwenzake wa India Rajnath Singh pamoja na maafisa wao wakiwa New Delhi, tarehe 27 Aprili 2023. Picha na Wizara ya Ulinzi ya India/kupitia REUTERS
Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu na mwenzake wa India Rajnath Singh pamoja na maafisa wao wakiwa New Delhi, tarehe 27 Aprili 2023. Picha na Wizara ya Ulinzi ya India/kupitia REUTERS

India na China zilitofautiana wakati wa mkutano wa mawaziri wao wa ulinzi siku ya Alhamisi kuhusu umuhimu wa kurejesha amani kwenye mpaka wao wenye mzozo ili kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili.

India ilisema urejeshaji katika eneo hilo ni muhimu katika kukuza uhusiano huo, wakati China inaona hali ya mpakani kuwa tulivu, serikali hizo husika zilisema katika taarifa zilizotolewa baada ya mkutano huo.

Mkutano kati ya Waziri wa Ulinzi wa India Rajnath Singh na mwenzake wa China, Li Shangfu, ulifanyika katika jiji la New Delhi, pembeni mwa mkutano wa waziri wa ulinzi wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai siku ya Ijumaa.

Hii ilikuwa ni ziara ya kwanza kwa waziri wa ulinzi wa China nchini India tangu mivutano iliposambaa baada ya mapigano ya mpakani mwaka 2020 yaliyosababisha vifo vya wanajeshi 20 wa India na wanne wa China. Mkutano wa mawaziri wa ulinzi ulifuatiliwa kwa makini ili kuona kama mawasiliano ya viongozi wa ngazi za juu yatasaidia kuziba kile kinachoitwa "ukosefu wa uaminifu" kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya India ilisema waziri Singh alikuwa "ameeleza bayana kwamba maendeleo ya uhusiano kati ya India na China yatanatokana na kuwepo kwa amani na utulivu katika mipaka."

Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China ilisema waziri Li alielezea hali iliyoko katika mipaka “kwa ujumla ni tulivu” Taarifa ya China ilisema "pande zote mbili zinapaswa kuliangalia suala hili katika mtazamo wa muda mrefu, kuweka suala la mpaka katika nafasi muafaka kuhusu uhusiano wetu wa nchi hizi mbili, na kuhimiza uhalalishaji wa hali ya mpaka haraka iwezekanavyo."

XS
SM
MD
LG