Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 23:14

Chama cha Wiper chasema Kalonzo Musyoka bado ni mgombea urais


Kalonzo Musyoka
Kalonzo Musyoka

Chama cha Wiper nchini Kenya kimewahakikishia wafuasi wake kiongozi wao Kalonzo Musyoka bado yuko katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Agosti 9, kinyume na ripoti za awali zilizoeleza kuwa amezuiliwa na Tume ya Uchaguzi, IEBC, kwamba alishindwa kutimiza baadhi ya masharti.

Chama Jumamosi kilitupilia mbali ripoti kwamba Kalonzo amezuiliwa kuingia katika kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu alishindwa kuwasilisha sahihi kwa njia ya elektroniki kwa IEBC.

“Bodi ya Taifa ya Uchaguzi (NWB) inataka kuthibitisha kwamba chama kimetimiza matakwa yote na tayari tumewasilisha nakala ya wafuasi wa mgombea wetu Mei 28, 2022 ambapo tumetimiza hayo kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na IEBC ambayo ni Mei 29, 2022,” taarifa ya Wiper ilisema.

IEBC Jumamosi, ilitoa orodha ya wagombea 16 wanaowania urais ambao wataingia katika awamu ijayo ya uteuzi ambayo inaanza Jumapili.

Kalonzo, ambaye alimtaja Andrew Sunkuli kama mgombea mwenza wake, alikuwa hayumo katika orodha hiyo hata baada ya kuwasilisha nyarakati zinazotakiwa na tume ya uchaguzi, zikiambatana na sahihi za wapiga kura walioandikishwa.

Mwenyekiti wa Wiper NEB, Agatha Solitei, hata hivyo, alitupilia mbali madai ya kuwa Kalonzo alizuiliwa katika ushindani huo wa kuwania nafasi ya juu ya uongozi katika nchi na kwamba maelezo yaliyotolewa hayakuwa sahihi.

“Bu muhimu kwa umma kufahamu kuwa habari zilizowasilishwa hazikuwa sahihi kwa vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Steven Kalonzo Musyoka hajapitishwa au amezuiliwa na IEBC kuwania urais wa Jamhuri ya Kenya,” taarifa ilisema.

XS
SM
MD
LG