Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 13:48

Wawili wauawa katika maandamano Burundi


Polisi wa Burundi katika juhudi za kuzuia maandamano Bujumbura
Polisi wa Burundi katika juhudi za kuzuia maandamano Bujumbura

Polisi nchini Burundi wameuawa waandamanaji wawili katika vurugu zilizozuka wakati mamia ya watu wakijaribu kuandamana Jumapili kupinga hatua ya chama tawala cha CNDD-FDD kumteuwa Rais Pierre Nkurunziza kuwania awamu nyingine ya uongozi katika uchaguzi wa Juni.

Shirika la Msalaba Mwekundu na mashahidi wanasema polisi walitumia mabomu ya machozi na maji wa kuwasha kutawanya watu waliokuwa wakielekea katikati ya Bujumbura kwa maandamano.

Chama tawala kilimteua rasmi Rais Nkurunzinza kugombania urais katika uchaguzi ujao katika mkutano mkuu wa chama Jumamosi mjini Bujumbura.

Uhalali wa Rais Nkurunziza kugombania tena urais unapingwa kutokana na maelezo ya kisheria kuhusu matumizi ya maneno katika makubaliano ya amani yaliyofikiwa Arusha Tanzania na katiba ya nchi hiyo.

Makubaliano ya Arusha yanasema rais asiwe madarakani zaidi ya mihula miwili. Lakini katiba ya 2005 inasema rais lazima achaguliwe kwa kura ya wingi wa watu. Katika awamu yake ya kwanza rais Nkurunzinza alichaguliwa na bunge sio wananchi – kwa hiyo wafuasi wake wanasema akigombania sasa ndio itakuwa awamu yake ya pili.

Wapinzani wanasema hata awamu yake ya kwanza alipochaguliwa na bunge inahesabika.

XS
SM
MD
LG