Wananchi wa Brazil wanaotetea demokrasia wamejitokeza kumuunga mkono Rais wao Luiz Inácio Lula da Silva baada ya baadhi ya wafuasi wa Rais wa zamani Jair Bolsonaro kuvamia majengo ya bunge, mahakama kuu na ikulu. Hata hivyo askari wa kuzuia ghasia waliweza kuwaondoa.