Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea bila ya viatu hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na mashuhuri wanaojulikana sana katika historia. Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram. Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi. Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.
Matukio
-
Januari 28, 2023
Russia yafanya mashambulizi 44 ya anga Ukraine
-
Januari 28, 2023
Je, Arsenal wanaweza kuwa wapinzani wa muda mrefu wa Manchester?
-
Januari 28, 2023
Sudan na Ethiopia wafikia makubaliano ya bwawa lenye utata
-
Januari 27, 2023
Waziri wa Fedha wa Marekani aipongeza Afrika Kusini kwa ujasiri wake