Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 07:56

BoT yaidhinisha Benki ya Twiga kuungana na TPB bank


Benki Kuu Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeziruhusu benki ya Twiga (Twiga Bancorp Ltd) na benki ya TPB (TPB Bank Plc) kuungana kuwa benki moja kuanzia Mei 17, 2018

Kwa mujibu taarifa ya BoT utaratibu huo umetangazwa Jumatano katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Dkt. Kibesse amesema benki ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi wa BoT kwa sasa imeunganishwa na benki ya posta na kwamba utekelezaji wa hatua hiyo unaanza mara moja Mei 17, 2018.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mali za wateja na madeni ya benki hiyo sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public Limited Company.

BoT, ambayo ina mamlaka ya kusimamia mabenki na taasisi za fedha kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, ilichukua usimamizi wa Twiga Bancorp kutokana na benki hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji.

Uamuzi huo wa kuziunganisha benki hizo ambazo zote zinamilikiwa kwa sehemu kubwa na Serikali ya Tanzania unahitimisha jukumu la BoT kusimamia uendeshaji wa benki ya Twiga tangu tarehe 28 Oktoba 2016.

“Muungano huu utaifanya Benki Kuu kusitisha usimamizi wa benki ya Twiga na mambo yote kuhusiana na benki hiyo yatafanywa na benki ya TPB kuanzia tarehe 17 Mei 2018,” alisema Naibu Gavana Dkt Kibesse katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG