Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:22

Bob Dole ametoa heshima za mwisho kwa Bush 41


Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush
Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush

Bob Dole mwenye miaka 95 alipiga saluti kwa mkongwe mwenzake wa vita vya pili vya dunia "Bush 41" kabla ya mazishi ya kitaifa Jumatano

Msururu wa waombolezaji waliendelea kutoa heshima zao kwa Rais wa zamani wa Marekani, George H.W. Bush kwa kuzunguka eneo maalumu ndani ya bunge la Marekani mahala lilipowekwa jeneza na kufunikwa bendera ya Marekani, siku moja kabla ya mazishi ya kitaifa ya rais huyo wa 41 Marekani.

Wageni wakiwemo wamarekani wa kawaida, watu ambao walihudumu nafasi mbali mbali wakati wa utawala wake, pamoja na wakurugenzi wa zamani na wa sasa wa idara ya ujasusi Marekani-CIA.

Seneta wa zamani Bob Dole akitoa heshima za mwisho
Seneta wa zamani Bob Dole akitoa heshima za mwisho

Miongoni mwao alikuwa kiongozi wa zamani wa walio wengi katika baraza la Seneti na pia mgombea wa zamani wa urais Bob Dole ambaye alifika katika eneo maalum la Capitol Rotunda akiwa kwenye kiti cha wagonjwa. Alipatiwa msaada wa kusimama na mara aliposimama vyema, Dole mwenye miaka 95 alipiga saluti kwa mkongwe mwenzake wa vita vya pili vya dunia. Jeb Bush mtoto wa kiume wa Bush 41 alituma ujumbe kwenye Twitter akimshukuru Seneta Dole.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania Trump walitoa rambi rambi zao kwa faragha kwa mtoto wa marehemu George H. W. Bush, ambaye pia alikuwa rais wa zamani wa Marekani George W. Bush rais wa 43 akiambatana na mkewe Laura Bush pamoja na wanafamilia wengine wa ukoo wa Bush wakiwa kwenye nyumba ya wageni wa Rais iitwayo Blair House iliyopo jirani na White House.

Kabla ya mkutano huo Melania Trump alimtembeza Laura Bush kuangalia mapambo ya sikukuu ya Christmass kwenye eneo la White House.

Rais Trump na mkewe Melania Trump
Rais Trump na mkewe Melania Trump

Rais Trump na mkewe Melania waliungana na waombolezaji wengine Jumatatu jioni huko Capitol Rotunda kutoa heshima zao kwa rais huyo wa zamani wa Marekani aliyefariki Ijumaa katika jimbo la Texas.

XS
SM
MD
LG