Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:44

Biden kusaini mswaada wa miundombinu wa dola trilioni 1


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatatu ameanda hafla kwenye Ikulu ya Marekani White House ambapo atatia saini mswaada wa miundombinu wa dola trillioni 1 ambao hatimaye ulipitishwa na Baraza la Wawakilishi baada ya miezi kadhaa ya mvutano.

Mswaada huo unapendekeza uwekezaji mkubwa kote nchini ili kushughulikia barabara na madaraja yaliyoharibika, kuboresha huduma ya reli na kupanua usafiri wa umma.

White House imesema hafla ya kutia saini mswada huo itajumuisha magavana na mameya kutoka vyama vya Democratic na Republican, vile vile viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyabiashara.

Mswada huo unajumuisha mabilioni ya dola kushughulikia mapungufu katika upatikanaji wa mtandao wa internet, haswa katika familia za watu wenye kipato cha chini, maeneo ya vijijini na jamii za makabila.

Pia kuna miradi ya kuimarisha mtandao wa umeme, pamoja na mifumo ya maji na maji machafu. Viwanja vya ndege vitaboreshwa, na kumeahidiwa pesa za kujenga vituo vya kuchaji magari ya umeme na kununua mabasi ya shule yanayotumia umeme, mafuta na nishati ya juwa.

XS
SM
MD
LG