Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 03:56

Maseneta wa Marekani waelezea dola trilioni moja mpango wa kuboresha miundombinu ya nchi


Jengo la bunge la Marekani ambapo mijadala ya bajeti ya miundombinu inafanyika(Foto: Elizabeth Frantz/Reuters)

Hayo yalikuja katika kikao adimu cha Jumapili na wabunge hivi sasa watapata fursa ya kutoa marekebisho ya mswaada huo wenye kurasa 2,700. Pendekezo hilo lilijitokeza kwenye majadiliano ya wiki kadhaa yaliyohusisha maseneta wa Democratic na Republican pamoja na White House

Maseneta wa Marekani wameelezea mpango wa pamoja wa matumizi ya miundombinu wa dola trilioni moja ili kurekebisha barabara na madaraja nchini Marekani na kupanua huduma za aina hiyo zilizozoroteka kwa nchi nzima.

Hayo yalikuja katika kikao adimu cha Jumapili na wabunge hivi sasa watapata fursa ya kutoa marekebisho ya mswaada huo wenye kurasa 2,700. Pendekezo hilo lilijitokeza kwenye majadiliano ya wiki kadhaa yaliyohusisha maseneta wa Democratic na Republican pamoja na White House.

Mfano wa dola ya Marekani
Mfano wa dola ya Marekani

Inajumuisha dola milioni 550 katika matumizi mapya pamoja na dola bilioni 450 katika pesa zilizoidhinishwa awali. Ikiwemo na kifurushi cha dola bilioni 110 kwa ajili ya barabara na madaraja, dola bilioni 39 kwa usafiri wa umma, na dola bilioni 66 kwa ajili ya reli.

Dola bilioni 55 zimetengwa kwa ajili ya maji ya kunywa na miundo mbinu ya maji taka pamoja na mabilioni ya viwanja vya ndege, bandari, mtandao wa internet na vituo vya kuchaji magari ya umeme.

XS
SM
MD
LG