Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:58

Biden kusaini mswada wa miundombinu


Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza baada ya mswada wa miundombinu kupitishwa na bunge
Rais wa Marekani Joe Biden akizungumza baada ya mswada wa miundombinu kupitishwa na bunge

Rais wa Marekani Joe Biden leo ameanda hafla kwenye Ikulu ya Marekani White House, ambapo atatia saini mswada wa miundombinu wa dola trillioni 1 ambao hatimae ulipitishwa na Baraza la wawakilishi baada ya miezi kadhaa ya mvutano.

Mswada huo unapendekeza uwekezaji mkubwa kote nchini ili kushughulikia barabara na madaraja yaliyoharibika, kuboresha huduma ya reli na kupanua usafiri wa umma.

White House imesema hafla ya kutia saini mswada huo itajumuisha magavana na mameya kutoka vyama vya Democratic na Republican, vile vile viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyabiashara.

Mswada huo unajumuisha mabilioni ya dola kushughulikia mapungufu katika upatikanaji wa mtandao wa internet, haswa katika familia za watu wenye kipato cha chini, maeneo ya vijijini na jamii za makabila.

Pia kuna miradi ya kuimarisha mtandao wa umeme, pamoja na mifumo ya maji na maji machafu. Viwanja vya ndege vitaboreshwa, na kumeahidiwa pesa za kujenga vituo vya kuchaji magari ya umeme na kununua mabasi ya shule yanayotumia umeme, mafuta na nishati ya juwa.

XS
SM
MD
LG