Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 18:12

Biden kuanza kupangua sera za Trump zisizo kuwa na manufaa


Rais mteule akiwasili kuapishwa katika nje ya Bunge la Marekani.
Rais mteule akiwasili kuapishwa katika nje ya Bunge la Marekani.

Wasaidizi wa Rais mteule Joe Biden wamesema kwamba atachukuwa hatua za haraka kuanza kupangua sera za Trump zisizo za manufaa kwa Marekani, ikiwemo kukabiliana na janga la virusi vya Corona, Pamoja na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais mteule anatarajiwa kusaini amri 15 za kiutendaji, muda mfupi baada ya kuapishwa kama rais wa 46 wa Marekani.

Kulingana na msimamizi wa habari katika white house Jen Psaki, Biden atasaini amri hizo za kiutendaji na ilani alasiri hii, saa za hapa Washington DC, akiwa white house, na kutaka mashirika kuchukua hatua za ushirikiano kufanikisha sera zake.

Maafisa wanatarajiwa kuhakikisha kwamba kila mtu anayeingia katika majengo au ofisi za serikali anavaa barakoa katika juhudi za kupambana na janga la virusi vya Corona.

Biden pia anatarajiwa kusitisha mchakato wa Marekani kujiondoa shirika la afya duniani WHO, kuirejesha Marekani katika makubaliano ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ya Paris, kutekeleza mabadiliko katika sera y auhamiaji, kusitisha ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico, kuondoa marufuku ya wasafiri kutoka nchi za kiislamu kuingia Marekani, miongoni mwa mengine.

XS
SM
MD
LG