Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:14

Trump amewaaga wananchi kwa njia ya video na kumtakia mema mrithi wake


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Trump alijisifia kwa kubuni uchumi bora katika historia ya Dunia. Anasema pia anajivunia kuwa rais wa kwanza katika miongo kadhaa ambaye hajaanzisha vita mpya

Rais Donald Trump ametoa video ya kuaga wananchi katika siku yake ya mwisho madarakani, akimuombea na kumtakia mafanikio mema mrithi wake M-Democratic, Joe Biden, lakini bila kumtaja jina lake.

Katika takribani dakika 20 za matamshi kwenye video hiyo ya Jumatatu, Trump alijisifia kwa kubuni uchumi bora katika historia ya Dunia. Anasema pia anajivunia kuwa rais wa kwanza katika miongo kadhaa ambaye hajaanzisha vita mpya.

Wakati video ilipotolewa na White House kwenye You Tube, ndege binafsi iliyombeba Rais mteule Joe Biden ilitua, katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Andrews Airforce Base, katika jimbo la Maryland, mahala ambako Trump anatarajiwa kuagwa kwa sherehe za mwisho Jumatano asubuhi, na baadae atapanda ndege yake ya rais kwa mara ya mwisho akielekea jimbo la Florida.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Trump anavunja utamaduni kwa kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Biden, ambaye alishinda kura za wananchi na kura za wajumbe katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3 mwaka jana.

Trump alitangaza madai yasiyo ya kweli kwamba kulikuwa na wizi katika upigaji kura, na tangu wakati huo hajampongeza Biden kwa ushindi alioupata.

XS
SM
MD
LG