Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 00:18

Besigye aomba ushirikiano wa Waganda wanaoishi nje.


Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Kampala, Uganda, Feb. 21, 2016.
Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Kampala, Uganda, Feb. 21, 2016.

Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye anawaomba raia wa nchi hiyo wanaoishi nje kuendelea kutoa msukumo wa demokrasia nchini Uganda.

“Nafikiri wana njia mbili au tatu. moja ni kuendelea na mazungumzo na serikali katika nchi wanazoishi na kuomba ushirikiano wao katika mazungumzo na utawala nyumbani na pia kuzungumza nasi ambao tunapinga utawala uliopo madarakani kwa muda mrefu “ Besigye aliiambia VOA kwa njia ya simu akiwa katika ziara fupi ya matembezi Uingereza ambako atazungumza na raia wa Uganda wanaoishi huko.

Anatarajia kusafiri baadaye mwezi huu kuingia nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG