Fedha hizo zitafadhili takriban megawati 106 (MW) yenye uwezo wa kuzalisha nishati ya jua yenye mifumo inayotumia nguvu ya betri na uhifadhi wa nishati na kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme wa maji wa MW 41.
Nchi hizo ni Sierra Leone, Liberia, Togo na Chad. Fedha hizo zitasaidia juhudi za usambazaji wa umeme.
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, ambaye aliongoza sherehe za utiaji saini siku ya Jumatano, alisema makubaliano hayo ni mwanzo wa mapinduzi ya usambazaji na upatikanaji wa nishati katika nchi husika.
Afrika Magharibi na Afrika ya Kati ina moja ya viwango vya chini sana vya usambazaji umeme ukichanganya na baadhi ya gharama kubwa sana za umeme barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Gharama za nishati zimeongezeka zaidi kwa sababu ya uvamizi wa Russia mnamo Februari 2022 nchini Ukraine, wakati bei za mafuta zimeongezeka.
Mpango wa pamoja wa nishati Afrika Magharibi, ni mwelekeo wa kikanda kuboresha umeme katika eneo hilo, na pia zitapokea baadhi ya fedha zilizo idhinishwa mwezi Desemba chini ya mradi mpya wa Benki ya Dunia wa Kikanda ulioanzisha juhudi za dharura za nishati ya jua.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.
Facebook Forum